WANAFUNZI WAANDAMANA KUFUATIA MGOMO WA WALIMU-KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/31/2012/15:07 Katika hatua inayoashiria kuwa hali inayosababishwa na mgomo wa walimu unaoendelea nchi nzima athari zake sasa zimefika mbali baada ya wanafunzi wa shule za msingi za Mailimoja na Maendeleo za mjini Kibaha kuandamana wakidai haki yao ya kufundishwa kama ilivyo ada. Wanafunzi hao ambao walikuwa wakijiongoza wenyewe huku wakipita barabara kubwa ya Morogoro wakiimba nyimbo za kudai haki ya kufndishwa na wakiitaka serikali iwalipe fedha walimu ambazo wanataka ili waweze kuendelea na masomo. ... Mmoja ya wanafunzi ambaye nimeongea naye amesema wameamua kuandamana baada ya kuona walimu wao wanasini halafu tena wanaondoka bila kwenda madarasani kama ilivyo ada. Kutokana na kadhia hiyo ilimbidi Diwani wa Kata ya Mailimoja kufanya kazi ya ziada akishirikiana na askari kata ili kujaribu kuwaongoza wanafunzi hao ambao walionekana kupagawa na kuchoka kutokana umbali mrefu waliotembea bila wahusika wa elimu wa kata au mji kujitokeza kuwaeleza neno lolot...