NAIBU WAZIRI AFYA ATAKIWA ASITISHWE NA LUGHA,DOCTOR NDIO MGANGA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/28/2015 2:41:35 PM
Serikali imetakiwa kuliangalia suala la tiba mbadala kwa umakini ili kuepusha upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusiana na tiba za asili na tiba mbadala katika kutibia magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa korofi kwa jamii.

Nimeongea na Mganga wa Tiba mbadala, DKT.BAHATI MAYALA ambaye ameeleza kusikitishwa kwake kwa hatua ya Waziri anayehusiana na afya, DKT.HAMIS KINGWANGWALA kuzuia waganga wa tiba mbadala kuacha kutumia neno DOCTOR ambalo ni lugha ya kigeni ambayo nayo inaamanisha mganga.

DKT.MAYALA amesema tendo linalofanywa na mganga wa hospitali la kusaidia watu kwa kuwaponya na magonjwa mbalimbali, ndivyo vivyo ambavyo mganga wa tiba mbadala anafanya katika kuhakikisha jamii haisumbuliwi na magonjwa ambayo yanaweza kutibika.

DKT.MAYALA ameishauri serikali kufanya ufuatiliaji kwa waganga wa tiba mbadala ambao wamekuwa wakijinadi kuwa na tiba za magonjwa mbalimbali ambayo yameshindikana hospitalini ili kujua madai yao ya kutibu magonjwa hayo wanao badala ya kujumlisha waganga wote na kuwadharau.

Aidha ameitaka serikali kutokuwa vivu katika kujua ukweli huo kuhusiana na tiba mbadala ikiwa sambamba na kuwateua wagonjwa amb ao watafanyiwa utafiti na waganga hao ikiwa pamoja na mkutoa ruzuku kwa wataalamu hao wa tiba za asili ili kuweza kuiponya jamii na maradhi ambayo yanweza kutibika na tiba asilia.

END



Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA