MISITU KUTUMIKA KWA UTALII
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/15/2015 1:15:09 PM
Shirika lisilo la kiserikali la usimamizi wa misitu ya asili ya
Tanzania imeanzisha mikakati mipya ya kuhakikisha misitu iliyopo ukanda wa Ruvu
Kusini inatumika kama kivutio cha watalii ili kuwezesha jamii inayozunguka
misitu hiyo kujua faida nyingine ya kutunza mazingira.
Akizungumza katika tukio la kimataifa la kitalii la kuendesha
baiskeli ndani hifadhi ya msitu Ruvu Kusini katika eneo la Kipangege Kisarawe,
Mratibu wa tukio hilo BW.YAHAYA MTONDA amesema kwa hatua hiyo wanajaribu
kuwajengea dhana wananchi ya faida zaidi ya misitu ya mbali ya mkaa na kuni.
BW.MTONDA ameongeza kwa kufanya hivyo itawezesha wanachi
kuilinda misitu hiyo kwa kujitoa na hivyo kuboresha suala zima la uboreshaji wa
mazingira, na hivyo kupunguza athari inayoletwa na hewa ya ukaa.
Naye mmoja wa washiriki wa mbio hizo za kimataifa za baiskeli
ambazo zimefanyika ndani ya hifadhi msitu wa Ruvu Kusini,ambaye pia ni mshauri
wa ufundi wa {TFCG} BW.ANDREW PERKIN ameeleza malengo ya kushiriki tukio hilo
ni kuwapatia wananchi uelewa wananchi juu ya umuhimu wa kulinda misitu ili
kuweza kufurahi mandhari nzuri ya uoto wa asili ambao unasababisha hali hewa
safi.
BW.PERKIN kwa upande wake
amesikitishwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kunakotokana na
ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa utunzaji mazingira.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wapanda Baiskeli (UWABA) BW.MEJA MBUYA amesema
kuwa wamekuwa wakihamasisha watu kupanda baiskeli kwani matumizi ya magari
yamekuwa yakiharibu mazingira kutokana na moshi unaotokanan na magari hayo.
Mbuya amesema kuwa mbali ya kupanda baiskeli wamekuwa wakitoa
elimu mbalimbali ya juu ya utunzaji wa misitu na kushauri matumizi ya nishati
ya jua na upepo katika baadhi ya matumizi ili kutoharibu mazingira. Jumla ya
watu zaidi ya 100 toka mataifa mbalimbali walishiriki tamasha hilo ambapo
walitembea umbali wa kilometa 30.
END.
Comments
Post a Comment