DK.MAGUFULI AOMBWA KUTANUA WIGO UTOAJI ELIMU BURE.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12/7/2015 10:54:19 AM
Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania DK.JOHN POMBE MAGUFULI ameombwa kutanua wigo wa
utoaji elimu bure kuanzia ngazi ya awali mpaka Chuo kikuu ili kutoa fursa ya
kupatikana kwa maendeleo kwa haraka.
Mkurugenzi
mtendaji wa shule ya awali ya MONTESSORI PRE-PRIMARY SCHOOL, BI. ANNE MASAKA
MAYOMBI ameyazungumza hayo wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo, ambapo
amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kukuza kiwango cha elimu nchini.
BI.MAYOMBI
ameongeza kuwa yeye kwa upande wake amefurahishwa na hatua ya kutangazwa kwa
utoaji wa elimu bure, ingawa amependekeza kuwa utoaji wa elimu kuambatane na
kuboresha maslahi ya Walimu.
Amehimiza
iwapo kama serikali itatoa ruzuku kwa shule za awali na kuwalipa Walimu ambao
wameamua kujiajiri baada ya kupata mafunzo ya Ualimu na kukosa ajira, suala
hilo litapata mafanikio makubwa.
Mgeni rasmi
katika hafla hiyo, Mchoraji maarufu wa katuni nchini, BW.MASOUD KIPANYA
akizungumza amesema wazazi wana wajibu wa kushirikiana na Walimu kuhakikisha
watoto wanapata elimu bora ambayo itawawezesha katika maisha yao ya baadaye.
BW.KIPANYA
amesikitishwa na risala ambayo imesomwa mbele yake kwa baadhi ya wazazi
kutowathamini watoto na hivyo kuathiri maendeleo ya elimu mtoto.
Hivyo
amewataka wazazi kubadilika na kuthamini watoto na walimu, na akasisitiza kama
unataka kulea Rais mzazi hana budi kumthamini mtoto kwani wao ndio viongozi na
Taifa la kesho.
END
Comments
Post a Comment