TGNP YAHIMIZA USHIRIKI SAWA KATIKA CHAGUZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/1/11/ 2015/ 2:38:54 PM
Waandishi wa
habari nchini wametakiwa kutoa elimu kuhusiana na ushiriki wa makundi ya
vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Hayo yamezungumzwa
na BI.REBBECA MJEMA kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya TGNP na kituo cha
sheria na haki za binadamu, katika mafunzo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu
j
uu ya ushiriki wa makundi ya wanawake,vijana na wenye ulemavu katika chaguzi
mbalimbali,
Bi.MJEMA
amesema imekuwa desturi kwa makundi hayo tajwa kuwekwa kando na kutopewa fursa
ya kushiriki katika kupata nafasi ya
kugombea katika chaguzi nchini, kutokana na baadhi ya wanasiasa kwa makusudi
kuyatumia makundi hayo kwa faida zao binafsi.
Mmoja waa
washiriki wa mafunzo hayo Mwandishi mwenye ulemavu wa macho kutoka Mkoa wa
Pwani, BW.ABDALLAH amesema yeye kwa upande wake alitumia haki yake ya kikatiba
kama Mtanzania ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali za mitaa,alikumbana
na changamoto mbalimbali ambazo kwa njia moja au nyingine zimekuwa kikwazo
kikubwa kwa watu kutoka kundi hilo kushiriki kikamilifu.
Bw. ABDALLAH
amebainisha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia kashfa,
matusi na kushambulia mtu binafsi badala ya kusema sera zao kama watawafanyia
nini wananchi, hali hiyo ilimkuta hata yeye alipobezwa na mgombea mwenzie
wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa,ambapo aliambiwa na mwenzake kuwa yeye
kutokana hali yake ya upofu hawezi kuwaongoza, na kusema ni ajabu ya mlemavu
kupata nafasi ya uongozi hali ambayo inapaswa kukemewa.
END.
Comments
Post a Comment