MGANGA WA KIENYEJI ATAPELI NA KUTISHIA KUUA
Ben
Komba/Pwani,Tanzania/Saturday, January 17, 2015
Mama mmoja
mkazi wa Picha ya ndege mjini Kibaha BI.SALMA RASHID amejikuta katika matata
makubwa kufuatia mtu aliyemwamini kumtunzia eneo lake kumdhulumu na kudai ni
lake na hati nalo.
BIBI SALMA RASHID mjane mweenye watoto watatu
katikam kipindi hicho yeye alikuwa anakabiliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo
na hivyo kulazimika kurudi nyumbani kwao Mkuyuni, Matombo Mkoani Morogoro.
Akiwa
anaendelea na tiba ndipo dada yake alipompa taarifa ya kuwepo kwa mganga mmoja
wa kienyeji maeneo hayohayo aliyetoka yeye angeweza kumtibia tatizo lake la
moyo kupeapea na kumfdahamisha jina la mganga huyo kama BW.ALLY HIYARI na
kumueleza kuwa anaweza kumsaidia tatizo lake hilo.
Katika
kipindi chote cha matibabu BIBI.SALMA RASHID alitokea kumwamini mganga HIYARI
na hivyo kumuelezea kuhusu yeye kumiliki eneo na kumtaka wakati yeye akiwa yupo
Morogoro kwa ndugu zake akijiangalia afya yake basi atupie macho katika eneo
lake kuepusha watu wengine kuvamia.
Lakini hata hivyo
hilo halikusaidia ndipo alipoibuka mtu mmoja askari akaanza ujenzi bila ridhaa
ya BIBI.SALMA RASHID, Na BW.HIYARI akampigia simu mmiliki halali wa eneo hilo
BIBI.SALMA ambaye alifika kutoka Morogoro na kwenda moja kwa moja kwa
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa BW.MWAIPOPO ambaye alichukua uamuzi wa kumuita
Yule mnunuzi wa kwanza na kumfafanulia ukweli kuwa eneo lile ni la BIBI.SALMA
RASHID, ingawa kesi hiyo ilifika Mahakama kuu na BIBI.SALMA kurudishiwa eneo
lake.
Katika
kipindi chote hicho, BW.ALLY HIYARI aliyepewa dhamana ya kusimamia eneo hilo
ilifikia wakati alitishia kumuua BIBI.SALMA RASHID, Pale mnunuzi wa kwanza
alipotaka kutoa fedha nyingine ili aweze kununua eneo lile kutoka kwa mmiliki
halali, kufuatia juhudi za upatanishi zilizofanywa na aliyekuwa mwenyekiti wa
kipindi hicho, BW.MWAIPOPO kumbe alikuwa na lengo la kuja kumzunguka baadaye
kama ilivyotokea.
Baada ya
mgogoro huo kwisha, BW.ALLY HIYARI alimtaka BIBI.SALMA RASHID amuuzie eneo lile
tokay eye amesaidia katika suala zima la ufuatiliaji wa kesi hiyo ikiwa
mahakamani, sasa ni shurti amakabidhi makaratasi ya umiliki kama zawadi nya
msaada aliompa.
Jambo hilo
alikumuingia akilini BIBI.SALMA RASHID na kumtaka,BW.ALLY HIYARI kutaja jumla
ya gharama anazodai katumia katika kumsaidia wakati kesi ikiendelea mahakama
kuu, aambazo zilikuwa hazifiki shilingi laki tatu,Kitu ambacho BW.ALLY HIAYRI
alikikataa na kuahidi kuwa angetumia njia ambvazo anazijua kuhakikisha anapata
umiliki wa eneo hilo,jambo ambalo halifanikiwa kwa kutumia fedha ambazo zilimsaidia
kuupotosha ukweli.
Kwa yupande
wake Mganga ALLY HIYARI alipofikiwa na RFA alipandwa na jazba huku akisema yeye
ndio mwenye eneo na hayupo tayari kujibu chochote juu ya eneo hilo ambalo
anadaiwa amedhulumu.
END
Comments
Post a Comment