SHERIA YA HAKI YA MTOTO 2009 ITEKELEZWE KWA VITENDO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/1/17/2015 2:12:19 PM
Shirika lisilo
la kiserikali la CENTRE FOR CHILDREN,YOUNG PEOPLE ADULT EDUCATION –CYDAD- la
mjini Kibaha limewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari kusaidia jamii
katika kuelewa sheria ya mwaka 2009 inayohusiana na haki ya mtoto.
Afisa mradi
wa shirika hilo, BI.MARGARETH ALOYCE amewaambia waandishi wa habari aliokutana
naomjini Kibah kujadiliana juu ya nafasi
ya vyombo vya habari na waandishi katika kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa
na jamii.
BI.ALOYCE
amesema kuwa kwa vyombo vya habari kutoa nafasi kwa habari zinazohusiana na
ukandamizaji unaofanywa kwa watoto kutasaidia kuipa mwamko jamii kuhusiana na
suala zima la haki za mtoto.
Ambapo
amebainisha kuwa vipaumbele juu ya utekelezaji wa sheria ya haki za mtoto ya
mwaka 2009, ni jamii iwekeze kuokoa uhai
watoto na wanawake,lishe, kuwawekea watoto mazingira rafiki mashuleni na
katika vituo vya afya, mtoto kuwekewa mazingira mazuri ya baadaye.
BIBI.ALOYCE
ameongeza ili mtoto apate ustawi haina budi kupewa elimu ambayo itamuwezesha
kuendesha maisha yake ya baadaye ikiwa pamoja na kuhakikisha usalama wa mtoto
anapokwenda na kurudi shuleni.
Akizungumza
katika majadiliano haya MWandishi wa habari wa DAILY NEWS, BI.IMELDA MTEMA
amesema kuwa mbali ya mchango kutoka kwa waandishi wa habari,ameitaka jamii
kuanzia sasa kuhakikisha mahali popote wanapokuwa katika mkusanyiko unaojumisha
watoto katika kuhakikisha haki zao zinazingatiwa.
Majadiliano
hayo ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa asasi hiyo kuhusiana na sheria ya
haki za mtoto ya mwaka 2009, ilifadhiliwa FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY, chini
ya uratibu wa UNICEF.
END.
Comments
Post a Comment