SHULE YA MSINGI MAILIMOJA YATIA AIBU KWA UBOVU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/20-01-
2015
Juhudi za serikali katika kuhakikisha inakuza kiwango cha elimu kwa
kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia inaonekana
kuwa ni ndoto ambayo ni zaidi ya ndoto ya Kimweri ambayo baadye
ilidhihirika kuwa ni bayana.

Hali ya shule ya msingi Mailimoja iliyopo katika ya halmashauri ya Mji
wa Kibaha inasikitisha kutokana na majengo yaliyopo shuleni hapo kuwa
kitisho cha uhai kwa Walimu na wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Mwandishi whabari hizi amezuru eneo la shule hiyo na kushuhudia shule
hiyo yenye wanafunzi 950, ikiwa na vyumba sita tu, viunavyotumika na
vine kati ya vyumba hivyo ambavyo vilijengwa na TASAF vikiwa chini ya
kiwango kiasi kwamba hata mkanda wa juu au GEBO haijawekwa.

Mwalimu Mkuu wa shule ya MSINGI Maili moja, BW.REGINALD FANUEL amesema
msongamano wa wanafunzi shuleni hapo ni changamoto kubwa wanayokuta
nayo na hivyo kuwalazimu Walimu kuwarundika wanafunzi katika vyumba
vichache vilivyopo.

BW.FANUEL ameongeza kuwa wamkuwa wakifanya juhudi mbalimbali za
kuimarisha shule hiyo ikiwa pamoja na kuwashirikisha wazazi kupitia
michango ambapo kila mzazi anatakiwa kuchangia shilingi 5000 ili
kufanya ukarabati mdogo katika madarasa ambayo yanatumika sasa.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya shule ya msingi Mailimoja, BW.SAID
CHITENJE amebainisha wakati yeye anaingia katika nafasi hiyo alikuta
shule hata vyoo ni shida na ndipo alipoitisha kikao cha wazazi na
kuwataka wachangie, na wazazi walifanya hivyo na kufanikiwa kupata
vyoo.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kamati ya shule, BW.CHITENJE
amesikitishwa na halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kushindwa kuongeza
nguvu hata maeneo ambayo wazazi wameshachangia kitu ambaco kinakatisha
tama na kuona shule hiyo kama imetelekezwa.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA