WAFANYABIASHARA WA MAZAO YA MISITU WANATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MALIASILI-VIDEO



Ben Komba/Pwani Tanzania/25-4-2014

Mtandao wa wasafirishaji na wafanyabiashara Kibaha MWAMMIKI wametakiwa kushirikiana na Idara ya maliasili, katika kuhakikisha wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na watu wanaojifanya ni wakazi wa idara hiyo.

Meneja wa misitu kanda ya mashariki inayojumuisha mkoa wa Morogoro na Pwani, BW.BAKAR SALIM MOHAMED amesema ni juu ya wafanyabiashara wa mazo ya misitu kutoa ushirikiano stahili kwa idara ya maliasili ili kuwezas kuwabana watu wanaojitishwa dhamana hiyo kinyume na sheria.

BW.MOHAMED amebainisha kuwa kumekuwepo na baadhi ya watumishi wa idara hiyo na baadhi ya maaskari kutumia doria zinazoendeshwa na maliasili kwa maslahi binafsi, kiasi cha kuwasumbua hata baadhi ya wafanyabiashara wenye vibali kwa kuwababaisha kwa lengo la kutaka kupewa kitu kidogo.

Meneja huyo wa misitu kanfda ya mashariki, BW.BAKAR MOHAMED amewataka wafanyabiashara hao kuwasiliana na maliasili inapotokea kukamatwa katika mazingira tatanishi,ili kuweza kujua uhalali wa kukamatwa nao na hasa ikizingatiwa kuna baadhi wanatumia fursa hiyo kudai rushwa badala ya nia ya kweli ya kulinda maendeleo ya misitu nchini.

Naye mfanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Kibaha, BW. ABDALLAH MATUMBO ambaye anajishughulisha na biashara ya kuni, kwa upande wake amesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

BW.MATUMBO amesema imekuwa kawaida kwa askari kuwasumbua hata kama nyaraka zote zimekamilika, lakini utakuta watasimamishwa barabarani kila baada ya hatua fulani hali inayosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara hao.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA