MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA-VIDEO
Ben
Komba-Pwani-Tanzania-25=4-2014
Kufuatia
mvua zinazoendelea kunyesha nchini, maiti tano zimepatikana zikielea katika Mto
Mpiji kufuatia kusombwa na maji walipokuwa wanajaribu kuvuka daraja
linalounganisha kati ya wilaya ya Kinondoni na halmashauri ya mji wa Kibaha.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa Lumumba,
BW.GIDEON TAIRO amethibitisha kuwatambua marehemu hao ambao ni BW.JAJI MNEMWA
na BW.MUSHI ambao walikuwa wanafanya shughuli zao za uzalishaji mjini Dar es
Saalam na ni wakazi wa eneo lake.
BW.TAIRO
ameongeza kuwa kwa kupatikana kwa miili kumesababisha idadi ya waliokufa na
maji katika mto Mpiji kufikia watano, wane wakiwa wanaume na mmoja mwanamke.
BW.TAIRO
amebainisha kuwa kwa muda mrefu wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiomba kujengwa
kwa daraja la kudumu katika eneo hilo ili liweze kupitika kipindi chote cha
mwaka na hasa ikizingatiwa linatumika na watu wa kada mbalimbali katika jamii,
hususan wanafunzi, wazee na kinamama wajawazito.
Naye Katibu
wa CCM tawi la Lumumba, BW.SHAMII BAKARI ambaye amesema kilio cha kuhitaji
kujengwa kwa daraja eneo hilo ni cha muda mrefu, pamoja na kufika kwa viongozi
mbalimbali wa chama cha mapinduzi.
BW. BAKAR
ameongeza kuwa Pamoja na eneo hilo kutembelewa na diwani na Mbunge wa Kibaha
mjini Kibaha, BW. SYLVESTER KOKA mpaka sasa hakuna kilichofanyika, ingawa
wananchi mpaka sasa wamejitahidi kutumia nguvu zao na kujenga nguzo tatu ambazo
zinatumika kama kinga ya miti iliyowekwa ili kuwezesha wananchi kuvuka eneo
hilo.
BW.BAKARI
ameitaka serikali kutupia macho daraja hilo ambalo ni kiungo kati Mikoa miwili
jirani kulitengeneza ili waweze kupita kwa usalama, na ikizingatiwa kuwa huduma
zote muhimu zinapatika upande wa pili wa Mkoa wa Dar Es Saalam.
END.
Comments
Post a Comment