WAFANYABIASHARA WA MAZAO YA MISITU WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MALIASILI
Ben
Komba/Pwani Tanzania/25-4-2014
Mtandao wa
wasafirishaji na wafanyabiashara Kibaha MWAMMIKI wametakiwa kushirikiana na
Idara ya maliasili, katika kuhakikisha wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa
na watu wanaojifanya ni wakazi wa idara hiyo.
Meneja wa
misitu kanda ya mashariki inayojumuisha mkoa wa Morogoro na Pwani, BW.BAKAR
SALIM MOHAMED amesema ni juu ya wafanyabiashara wa mazo ya misitu kutoa
ushirikiano stahili kwa idara ya maliasili ili kuwezas kuwabana watu
wanaojitishwa dhamana hiyo kinyume na sheria.
BW.MOHAMED
amebainisha kuwa kumekuwepo na baadhi ya watumishi wa idara hiyo na baadhi ya
maaskari kutumia doria zinazoendeshwa na maliasili kwa maslahi binafsi, kiasi
cha kuwasumbua hata baadhi ya wafanyabiashara wenye vibali kwa kuwababaisha kwa
lengo la kutaka kupewa kitu kidogo.
Meneja huyo
wa misitu kanfda ya mashariki, BW.BAKAR MOHAMED amewataka wafanyabiashara hao
kuwasiliana na maliasili inapotokea kukamatwa katika mazingira tatanishi,ili
kuweza kujua uhalali wa kukamatwa nao na hasa ikizingatiwa kuna baadhi
wanatumia fursa hiyo kudai rushwa badala ya nia ya kweli ya kulinda maendeleo
ya misitu nchini.
Naye
mfanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Kibaha, BW. ABDALLAH MATUMBO ambaye
anajishughulisha na biashara ya kuni, kwa upande wake amesema wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya
kila siku.
BW.MATUMBO
amesema imekuwa kawaida kwa askari kuwasumbua hata kama nyaraka zote
zimekamilika, lakini utakuta watasimamishwa barabarani kila baada ya hatua
fulani hali inayosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara hao.
END.
Comments
Post a Comment