KWAYA YA MTAKATIFU DON BOSCHO YAFANYA HARAMBEE.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-01-2014/12:28 Jumla ya shilingi Milioni tatu zimepatikana katika harambee ya kuiwezesha kwaya ya MTAKATIFU.DON BOSCHO ya mjini Kibaha katika Mkoa wa Pwani kuweza kufanya ziara yake katika mji wa Namugongo nchini Uganda kwa ajili ya ziara ya Kitume. Akizungumza wakati wa harambee iliyofanyika katika ukumbi wa TRIPPLE J, Katibu wa kwaya MTAKATIFU DON BOSCHO, BI.PHILOMENA SHIJA amesema lengo la kuaandaa harambee hiyo ni kutafuta shilingi milioni 25 kwa ajili ya safari ya Namugongo, Uganda. BI.SHIJA ameongeza kuwa mbali ya kutafuta nauli ya kwenda Uganda, harambee hiyo pia ilikuwa na jukumu la kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa basi ambalo litawawezesha kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine lenye thamani ya shilingi milioni 70. Katibu huyo wa Kwaya ya MTAKATIFU DON BOSCHO,. Bi.PHILOMENA SHIJA amebainisha kwa hiyo ambayo ina miaka 30 kutoka kuanzishwa kwake, mpaka sasa imetoa albamu sita. Naye Mgeni Rasmi katika hafla hi...