ABAKA MTOTO WA MIAKA 3
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2012 6:41:51 PM Mtoto mdogo anayesoma shule ya chekechea mwenye umri wa miaka mitatu na miezi minane amebakwa leo jioni hii na kijana aliyejulikana kwa jina moja la JUSTIN mwenye umri wa miaka 20 na kusababishiwa maumivu makali katika maeneo ya Mpakani mjini Kibaha. Kwa mujibu wa mzazi wa mtoto BIBI. ASHURA WAZIRI amesema kama kawaida mtoto wake alirudi shule , na akambadilisha nguo na akaenda kucheza na mwenzake, wakati akicheza huku kijana yule mbaya JUSTIN alikuwa anafua nguo zake uwani katika nyumba hiyo ya kupanga. JUSTIN ambaye anafanya kibarua cha kuchoma kuku eneo la Maili Moja majira ya jioni, inasemekana hana hata miezi miwili toka alipowasili kutoka Mkoani Iringa, mtoto huyo kama mtoto mwingine yoyote alikuwa na upendo na wapangaji wengine wote hivyo kuingia chumba kimoja hadi kingine kwake ilikuwa kawaida. Lakini tofauti na siku nyingine mtoto huyo aliingia chumbani alichokuwa analala JUSTIN huku Mama yake akiwa dukani ambako amejiajiri hak...