Posts

ZAO LA UYOGA MKOMBOZI KWA WAJASIRIAMLIA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13:21/25-07-2013 Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwekeza katika zao la uyoga ili waweze kujiongezea kipato, katika suala zima la kukabiliana na maskini miongoni mwa jamii. Akiongea katika mafunzo yanayohusiana na kilimo cha zao la uyoga, Mtaalam PETRO MATHEW amebainisha kuwa iwapo wajasiriamli wakiamua kujikita katika kilimo cha zao wataweza kufaidika kiafya na kiuchumi. BW.MATTHEW amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapatia mbinu na utaalamu wa kufanikisha uoteshaji wa uyoga katika mazingira ya nchi ya Tanzania, ambapo pia uzalishaji wake unasaidia kuweka mazingira katika hali safi, kutokana na kilimo chake kutumia zaidi takataka. Mtaalamu huyo BW.MATTHEW ameongeza kuwa uyoga ustawi katika takataka ambazo hazijaoza,takataka zilizooza kidogo na hata takataka zilizooza kabisa na hivyo kusababisha matumizi ya takataka kuchukua nafasi kubwa katika uzalishaji wa zao hilo. BW.MATTHEW ameelezea faida za uyoga ni pamoja na kuongeza kinga za mw...

MSASA POLISI JAMII.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013 Wananchi wametakiwa kutumiaulinzi shirikishi jamii kujiletea amani na utulivu katika maeneo kunakosababishwa na watu wanaoishi nao mtaani kwa kutoa taarifa katika suala zima la kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao. Mkuu wa Jeshi la Polisi mjini Kibaha, Mrakibu wa Polisi BAKARI KAWINGA amesema hayo wakati alipokutana na polisi jamii katika kata ya Pangani ambapo amefurahishwa kwa Kata hiyo kuwa na matukio kidogo ya uhalifu, kulinganisha na kabla ulinzi huo haujanzishwa. BW.KAWINGA amebainisha kuwa iwapo umebahatika kuwa Polisi jamii, basi ni vyema kutumia fursa hiyo katika kutenda haki bila kubugudhi wengine kwa kisingizio cha kuwa na namba za simu za wakuu wa Jeshi hilo wa Mkoa wa Pwani. BW.KAWINGA ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lina nia njema ya kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na wananchi ambao watakuwa na wajibu wa kutoa taarifa wanapoona kuna jambo la kutia mashaka katika mitaa yao. Aidha ...

MAFUNZO YA UREFA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.

SKAUTI WAAPISHWA KIBAHA.

MASKAUTI ST.DON BOSCHO WAAPISHWA Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:36 Maskauti nchini wametakiwa kuenenda na maisha ya uskauti katika kipindi cha maisha yao yote ili waweze kuishi maisha ya ukakamavu utii na unyenyekevu ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii. Ameyaongea hayo Padri.FULGENCE RUTATEKURURWA wakati wa uapishaji wa maskauti kutoka shule ya ST.DON BOSCHO mjini Kibaha na kuhudhiriwa na maskauti wenzao kutoka nchini USWISSI. PADRI.RUTATEKURURWA amewataka maskauti hao kuishi maisha ya kiskauti na kuwa changamoto kwa wenzao,ili waweze kujiunga na skauti hivyo ni fursa waliyopewa kama maskauti wapya kuhamasisha wenzao kujiunga nao. Na amewataka kuambatana na kiapo chao ili waweze kutoa huduma hiyo kwa kufuata kanuni na miongozo ya skauti aidha amewakumbusha mara mtu unapokuwa skauti basi unakuwa skauti milele. Naye Kamishna msaidizi wa skauti mkoa wa Pwani, Skauta ANTHONY MWENDA  Amesema lengo la hafla hiyo ni kuapisha maskauti wapya wa ST.DON BOSCHO ambao...

BONANZA LA MICHEZO KWA WANAWAKE KKKT.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:06 Wanawake wakristo nchini wamehimizwa kushiriki Bonanza la michezo  kwa wanawake wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambayo itakuwa inafanyika kila baada ya klipindi Fulani katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo, BIBI. VERONICA KILEO amesema kuwa ni mara yao ya kwanza kuandaa bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha kinamama washiriki michezo. BIBI.KILEO amefafanua kuwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo ina kanda za kiusharika sita ndio zilizotakiwa kushiriki mashindano hayo lakini hata hivyo ni kanda nne tu zilizoshiriki Bonanza hilo, na kanda mbili za Zanzibar na magharibi zikishindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali. BIBI.KILEO ameongeza kuwa michezo mbalimbali imeshindaniwa katika bonanza hilo ikiwa pamoja na mazoezi kupasha mwili moto (warmup) kwa takriban dakika 15,kukimbiza kuku, kuvuta kamba na mpira wa pete. Mshauri wa kamati ya maandalizi ya Bo...

KATIBU CCM AONYESHA UKOMAVU WA KISIASA.

KATIBU CCM KIBAHA MJINI ASHANGILIWA NA BAVICHA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/10:27 Katibu wa Chama cha Mapinduzi mwishoni mwa wiki amejikuta akipigiwa makofi na wananchama wa chama cha maendeleo na demokrasia wa mjini Kibaha baada ya kujitokeza na kusuluhisha mvutano uliopo wa kuzuia CHADEMA kufungua matawi katika maeneo mbalimbali mjini Kibaha. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia Katibu wa CCM Kibaha mjini, BIBI.MWAJUMA NYAMKA akitoka ofisini kwake akaenda moja kwa moja kwenye kundi la vijana wa CHADEMA ambao katika kipindi hicho walikuwa wanavutana na Diwani wa CCM kata ya Mailimoja, BW.ANDREW LUGANO ambaye alikuwa akizuia ujenzi huo. Ambapo BIBI.NYAMKA kwa kutumia busara nadra sana kuonyeshwa na viongozi wa kisiasa, alimtaka diwani huyo kuwaacha waendele kufungua matawi kwani kinachoangaliwa na wananchi ni sera sio wingi wa matawi. Naye Diwani wa Kata ya Maili moja kupitia tiketi ya CCM, BW.ANDREW LUGANO yeye kwa upande wake amezuia ujenzi holela wa matawi ya C...

HABARI ZA POLISI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   Kibaha tarehe 19 Julai, 2013 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwani imemuhukumu Bw. Amosi Mwita Chacha umri miaka 40, Mkazi wa Miembe Saba Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwenda jela miaka 6 baada ya kukutwa na hatia katika Kesi ya Wizi wa vocha za tigo pamoja na kesi ya Kukutwa na Mihuri bandia. Mtuhumiwa huyo amekutwa na hatia kwa makosa yote mawili yaliyokuwa yakimkabili Katika kesi iliyokuwa ikisikilizawa na Hakimu Mkazi, Mhe. Aziza Mbadyo. Mwendesha mashitaka wa Serikali Bw. Emmanuel Maleko   ameeleza mbele ya   mahakama kuwa mtuhumiwa mnamo tarehe 03 Juni 2013 huko eneo la Sinza Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam alikutwa akiwa na Mihuri ya Afisa Mtendaji Mtaa wa kwesimu pamoja na wa Kituo cha Ukaguzi wa Maliasili cha Soni kilichopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mihuri hiyo katika usafirishaji wa mali asili kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam kwa ...