Posts

BABA ATELEKEZA FAMILIA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, April 11, 2012/.06:48:08 PM Mama mmoja mkazi wa mjini Kibaha BI. DIGNA LAURENT MASHAKAhivi karibuni amekumbwa na kisanga cha kutelekezewa watoto na mali za familia kuuzwa na mume wake wa ndoa, kwa sababu ya ndoa yao kuingiliwa na Mama mmoja mjane mkristo wa TAG anayejulikana kwa jina la Mama BETTY ambaye awali alikuwa anadai ana undugu na Mume wa mlalamikaji lakini kumbe ni kinyume chake. BI. DIGNA MASHAKA amebainisha mgogoro ulianza kwa yeye kuitwa mchawi na mume wake, na katika madai yake hayo siku moja mumewe BW. LAURENT MASHAKA (Michuzi) alirudi nyumbani na kumwita aende chumbani na mara alivyoingia akaanza kumkaba kiasi cha majirani kujitokeza na kuja kumuamulia, huku akidai ameweka uchawi kwenye viatu vyake na hivyo kumsababishia kupata fangasi. Na kutokana na tukio hilo BI.DIGNA MASHAKA aliamua kufungua kesi ya dhidi ya mume wake akilalamikia kitendo kilichofanywa naye, na lengo sio kuachana na mumewe, lakini kesi hiyo iliendeshwa kw...

BAJETI YA HALMASHAURI WILAYA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, 10 April, 2012/6:46:32 PM Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013 halmashauri ya wilaya ya Kibaha imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ni shilingi bilioni 12 ndizo zitakazotoka serikali kuu. Hayo yamesemekana katika kikao maalum cha bajeti cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kibaha, wakati Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, BW. CHRISTOPHER MDUMA alipokuwa anawasilisha makisio na makadirio ya mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka 2012/2013. BW.MDUMA amesema kati ya fedha hizo ambazo zimeanishwa katika bajeti hiyo, shilingi bilioni 2.5 ikiwa ni makusanyo ya ndani na ikiwa pamoja na michango ya jamii na nguvukazi yao ikiwa zaidi ya shilingi bilioni 10. BW. MDUMA akizungumzia upande wa mishahara amefafanua zaidi ya shilingi bilioni 8 zimetengwa upande huo, na matumizi ya kawaida yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.8 na miradi ya maendeleo ikiwa imetengewa shilingi bilioni 3.6. Awal...

MTENGEZA GOBOLE MBARONI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, 05 April, 2012/05:03:05 PM Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ERNEST MANGU ametoa wito kwa wataalam ambao wana uwezo wa kutengeneza bunduki kujitokeza hadharani ili kufuata taratibu za kisheria ili kuepuka mkono wa sheria badala ya kufanya kazi zao kwa kificho hali ambayo inaongeza wimbi la wizi wa kutumia silaha. Kamanda MANGU amesema kwa mtu yoyote ambaye anajua ana uwezo wa kutengeneza bunduki kuwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri aliyopo ili kupatiwa kibali ambacho kitamtambulisha kisheria kuhusika kwake kwa kazi hiyo, na vibali hivyo watawjibnika kuvilipia kila mwaka kama sheria inavyoelekeza na hivyo kuepusha uwezekano wa wataalamu hao kutmika sivyo na wahalifu. KAMANDA MANGU ameyazungumza hayo kufuatia kugundulika kwa kiwanda mwitu cha kutengeneza silaha kilichokuwa kikimilikiwa na BW. PETRO MAZIKU, katika eneo Mamdikongo kitongoji cha TABORA wilayani Mkuranga, ambapo mkazi huyto alikutwa na bunduki aina ya magobole yanayokaribia...

RIPOTI YA MTOTO ALIBAKWA YATHIBITISHA NDIVYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/1/2012 6:44:26 PM Taarifa ya daktari kuhusiana na tukio la kubakwa kwa mtoto wa mwenye umri wa miaka 3 na miezi minane ambalo limetokea March 27 mwaka huu imeshatolewa na kuthibitisha kuwa ni kweli mtoto huyto alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na miaka zaidi ya 20. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mama wa mtoto huyo, BI. ASHURA WAZIR amesema majibu hayo ambayo yanafuatiwa uchunguzi uliofanyika katika Hospitali teule ya mkoa ya Tumbi. Na kwa mujibu wa vyeti hivyo ambavyo mwandishi wa habari hizi ameviona vinaonyesha kuwa mtoto huyo amekutwa na michubuko meneo ya siri, damu na mbegu mbichi za kiume zinaaokadiriwa gramu 1. Cheti hicho namba:MFM 40 na namba ya uandikishaji 004 kilichotolewa hospitali ya Tumbi, kimeonyesha pia dawa alizopewa mtoto baada ya msukosuko huo ni PANADOL, Akashauriwa kuogea DETTOL, Erythromycin na kutakiwa kuhudhuria kituo cha kupima UKIMWI na kumuona mganga bingwa wa magonjwa ya kina...

ABAKA MTOTO WA MIAKA 3

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2012 6:41:51 PM Mtoto mdogo anayesoma shule ya chekechea mwenye umri wa miaka mitatu na miezi minane amebakwa leo jioni hii na kijana aliyejulikana kwa jina moja la JUSTIN mwenye umri wa miaka 20 na kusababishiwa maumivu makali katika maeneo ya Mpakani mjini Kibaha. Kwa mujibu wa mzazi wa mtoto BIBI. ASHURA WAZIRI amesema kama kawaida mtoto wake alirudi shule , na akambadilisha nguo na akaenda kucheza na mwenzake, wakati akicheza huku kijana yule mbaya JUSTIN alikuwa anafua nguo zake uwani katika nyumba hiyo ya kupanga. JUSTIN ambaye anafanya kibarua cha kuchoma kuku eneo la Maili Moja majira ya jioni, inasemekana hana hata miezi miwili toka alipowasili kutoka Mkoani Iringa, mtoto huyo kama mtoto mwingine yoyote alikuwa na upendo na wapangaji wengine wote hivyo kuingia chumba kimoja hadi kingine kwake ilikuwa kawaida. Lakini tofauti na siku nyingine mtoto huyo aliingia chumbani alichokuwa analala JUSTIN huku Mama yake akiwa dukani ambako amejiajiri hak...
Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2012 5:05:02 PM Chama cha waandishi wa habari wa mazingira na za watu wenye ulemavu Mkoani Pwani, (PEDWA) wamekutana leo kwa mara ya kwanza katika kupanga mkakati wa kuanza baadhi ya shughuli zake kwa kutumia nguvu zake yenyewe ili kuonyesha umuhimu wa masuala ya mazingira na ya watu wenye ulemavu katika jamii. Katika kikao cha pamoja na baadhi ya wadau wa masuala hayo, Mwenyekiti wa PEDWA- PWANI ENVIROMENTAL AND DISABLED WRITERS ASSOCIATION, BW. BERNARD KOMBA amesema lengo la kuanzishwa kwa asasi hiyo isiyo tengeneza faida, ni kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuthamini watu wenye ulemavu. BW. KOMBA amebainisha kuwa jamii bado inafanya dhihaka juu ya masuala hayo ambayo kuyatekeleza ni sawa na kutekeleza hqaki za msingi za binadamu, hasa ikizingatiwa binadamu wana haki ya kuishi katika mazingira yatakayomwezesha kufanya shughuli zake bila kusumbuliwa na majanga ya asili yanayosababishwa na ukataji misitu holela...
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2012 5:05:02 PM Chama cha waandishi wa habari wa mazingira na za watu wenye ulemavu Mkoani Pwani, (PEDWA) wamekutana leo kwa mara ya kwanza katika kupanga mkakati wa kuanza baadhi ya shughuli zake kwa kutumia nguvu zake yenyewe ili kuonyesha umuhimu wa masuala ya mazingira na ya watu wenye ulemavu katika jamii. Katika kikao cha pamoja na baadhi ya wadau wa masuala hayo, Mwenyekiti wa PEDWA- PWANI ENVIROMENTAL AND DISABLED WRITERS ASSOCIATION, BW. BERNARD KOMBA amesema lengo la kuanzishwa kwa asasi hiyo isiyo tengeneza faida, ni kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuthamini watu wenye ulemavu. BW. KOMBA amebainisha kuwa jamii bado inafanya dhihaka juu ya masuala hayo ambayo kuyatekeleza ni sawa na kutekeleza hqaki za msingi za binadamu, hasa ikizingatiwa binadamu wana haki ya kuishi katika mazingira yatakayomwezesha kufanya shughuli zake bila kusumbuliwa na majanga ya asili yanayosababishwa na ukataji misitu holela. Aidha kwa up...