MADAWA YA KULEVYA KILO NNE YAKAMATWA PWANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/28/2015 Jeshi la Polisi Mkoani Pwani umekamata kilo nne za unga unaosadikiwa kuwa madawa ya kulevya katika maeneo ya Kibaha kwa Mathias, katika halmashauri ya mji wa Kibaha. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao kutajwa kuhofia usalama wao, Mmoja wao amebainisha kuwa unga huo ulikamatwa majira ya saa tatu usiku kufuatia msako wa kumatafuta mtuhumiwa KANONI KAFU KANONI ambaye amekiuka masharti ya dhamana ya kesi mbalimbali zinazomkabili. Baada ya Polisi kufika katika eneo la tukio wakiongozwa na Afisa upelelezi ALLY MASIMIKE kutoka kituo cha Polisi cha Tumbi, mtuhumiwa katika mazingira yasiyoeleweka alifanikiwa kukimbia na kuwaachia Polisi na wadhamini waliotega mtego wa kumkamata nyumba. Na ndipo kufuatia hali hiyo ndipo Polisi wakaanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kupata BRIEF CASE ambayo ilikuwa na unga kilo nne, na waligundua unga huo walipofika kituoni Tumbi na kufungua mbele ya walalamikaji ambao walimdhamin...