Posts

Showing posts from December, 2014

ZIKO WAPI SIASA SAFI!!!?

Nasemaje ifike wakati kazi ya siasa ipewe heshima yake,sio sehemu ambayo magaidi,wahuni wanaweza kukimbilia,kwani kuna watu wenye akiba kubwa ya fedha wanataka kuvuruga amani ya nchi kama ilivyojitokeza kwenye uchaguzi wa TAMISEMI,wanasiasa wanachochea vijana kufanya vurugu,why? Au kwa kuwa wewe tajiri utapanda ndege mbio Ulaya na kutuachia kizaazaa hatutaki siasa hizo kama vp acheni siasa,vyombo vya dola msiwacheke watu wa dizaini hii,kwani nanyi familia zenu zitateseka. Like · · Share

HUJUMA,UBABE,UZEMBE VYATAWALA UCHAGUZI,TAMISEMI LAWAMANI.

Vitendo vya utekaji wagombea,kumwagiwa asidi ni vitendo vilivyojitokeza ktk uchaguzi huu, Ambapo baadhi ya maeneo kama wilayani Mafia vituo vingine vilikuwa havina peni kwa ajili ya kuendesha zoezi hilo. Wilayani mkuranga uchaguzi haukufanyika kutokana na vituo kutofunguliwa. BAGAMOYO vurugu zimezuka ktk kata ya vigwaza baada ya mgombea wa ccm kubwagwa. Napo mjini kibaha mtaa wa viziwaziwa wagombea wawili wa chadema wametekwa nyara usiku wa kuamkia uchaguzi. Kwa ujumla tamisemi hawana budi kubeba lawama kwa kuharibu zoezi kutokana na uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.

ALA NJAMA KUUA

12-Dec-14 12:22:35 AM-Tanzania/ Katika hali inayoashiria kuwa Dunia ya sasa imani imekwisha, wakazi wawili wa kijiji cha Soga halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameokoka kutoka katika mteggo wa kuuwawa kutokana na kuwa tishio kwa maharamia wa ardhi katika kijiji hicho. Mmoja wa watu  waliotaka kuuwawa ambaye ni Meneja wa shamba la ALAVI ESTATE linalomilikiwa na MOHAMED ENTERPRISES amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Kongowe na kuelezwa kuwa kuna watu wanakula njama ya kutaka kumuua. Bw.AMIR ameongeza kuwa sababu kubwa ambayo ilitaka kugharimu maisha yake ni mmoja wa maharamia wa mashamba, BW.RAMADHAN RASHID ambaye amejipata yupo katika kibano kufuatia kujishuhulisha na uuzaji wa mashamba ya ALAVI ESTATE, na hivyo  ili kuficha uvundo huo ndipo alipokula njama ya kukodi watu kuwauwa ambao anaona ni kikwazo katika azima yake hiyo. Naye mtu mwingine ambaye alikuwa kati ya watu waliotakiwa kuuwawa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti w...

RIDHIWAN ATAKA WANANCHI KUZINGATIA AMANI

Image
[Edit] < >       RIDHIWAN AHIMIZA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI Saturday, 6 December, 2014 0:52   Mark as Unread   Flag this message From:  "Bernard Komba" <kombabernard@yahoo.co.uk> To:  rfanewsroom@yahoo.com "MATUKIO GOOGLE" <matukio@googlegroups.com> Bcc:  "gazeti la kenya" <sundaynation@nation.co.ke> "VOICE NEWS" <africatv@voanews.com> Full Headers   Printable View Ben Komba/Pwani-Tanzania Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, BW.RIDHIWAN KIKWETE amewataka wapiga kura katika Jimbo la Chalinze kuwa watulivu kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji. Ameyazungumza hayo wakati akiongea na halmashauri ya Jimbo la uchaguzi Chalinze CCM, BW. KIKWETE amesema ni jambo bora kwa wananchi kuhudhuria katika mikutano ya kampeni ili kupata fursa ya kupima sera za kila chama. BW. KIKWETE amewaambia wajumbe wa kikao ...

WABABA WAASWA KUACHA KUNYEMELEA WANAFUNZI WA KIKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania Naibu mkuruigenzi elimu ya sekondari, TAMISEMI, BI.PAUKLINE NKWAMA amewataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kuhakikisha watoto wa kike wanapatiwa nafai ya kujiendeleza kielimu ili kuweza kuwakwamua na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. BI.NKWAMA ameyazungumzia hayo wakati wa kikao cha Mkutano mkuu wa kiwilaya wa shirika lisilo la kiserikali linalosaidia katika utoaji usaidizi kwa watoto wa kike wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaishala CAMFED. BI.NKWAMA ameongeza lengo la wadau kukutana kama walivyokutana hapo ni kujaribu kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kujitokeza katika upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata maendeleo binafsi na   familia zao. Amewataka wanafunzi wanaopatiwa usaidizi na shirika hilo la CAMFED {CAMPAIGN FOR FEMALE EDUCATION} kutumia msaada huo wa kielimu katika kuhakikisha wanajiendeleza zaidi katika suala zima la kuwa na mais...

MKUU WA MKOA WA PWANI ATAKA BARABARA ZITUNZWE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/desemba 4 2014 Mkuu wa mkoa w Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ameitaka wakala wa barabara mkoani hapa kuhakikisha wanaweka vibao kuainisha vivuko kwa ajili ya binadamu mifugo na uzito wa magari yanayotakiwa kupita njia husika. BIBI.MAHIZA amesema hayo katika Kikao cha Bodi ya barabara cha mkoa wa Pwani chenye lengo la kutathimini maendeleo ya miundombinu ya barabara, ambapo amesema kutokuwepo na vibao vinavyoashiria magari ya uzito gani yanatakiwa kupita barabara gani. Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwa kutozingatia utaratibu huo wa kuonyesha uzito wa magari yanayotakiwa kupita njia husika badala ya kufuata utaratibu wa kuhakikisha limebeba mzigo wa aina gani, ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa barabara zetu. Ametoa mfano wa Barabara ya lami ambayo imejengwa hivi karibuni na halmashauri ya mji wa Kibaha ambayo kwa sasa inaharibika kwa kasi kutrokana na magari yaliyozidi uzito kupita katikabarabara hiyo na kusasbabisha baadhi ya maeneo kubonyea na ...

MKANGANYIKO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA PWANI,Kama sms hii inavyojieleza

MH.KATIBU WA MKUU WA MKOA wananchi wa k.t.ngnji cha vundumu mtaa wa MBWEWE k.j.j. cha TARAWANDA .W. BAGAMOYO. HAWAJAJIANDIKISHA kwa kupiga kura kituo chao kiriaza mwaka 2000.Kituo hicho je?KIMEFUTWA?Kuna wapigakura zaidi ya [300] AMBAO hawakupata haki YAO .MH.TUNAOMBA UTUSAIDIE TATIZO HIRI ASANTE SANA kwaniaba ya wananchi.DAUDI.N.SITIMA.MW.K.TAWI.MBWEWE