CCM WAVUANA NGUO KIBAHA.
Ben Komba/PWANI-TANZANIA/22-05-2014/14:13
Chama cha mapinduzi Kata ya Mailimoja kinaingia katika
uchaguzi mdogo kujaza nafasi ya Katibu mwenezi wa Kata hiyo, kufuatia
kuondolewa kwa aliyekuwa anashikilia
nafasi kwa tuhuma mbalimbali.
Kutrokana na kuondolewa Katibu Mwenezi wa awali,
BW.SEBASTIAN MAGANGA ambaye kwa sasa amebadilisha makazi kuylisababisha nafasi
hiyo kuwa wazi na hivyo kukilazimu chama kutisha ucahaguzi mdogo.
Ambapo wagombea watatu wamejitokeza kugombea nafasi
hiyo ambao ni BW. LAZARO RIZIKI KULIGWA, BI. ASHURA SEKELELA na BW. JACOB ambao
ewanatarajiwa kupambana katika uchaguzi ambao utafanyika jumapili Mei 25.
Mmoja wa wagombea ambao nimeongea nao, BW.LAZARO
KULIGWA amesema yeye kwa upande wake ana uzoefu wa kutosha katika shughuli za
chama na ana uhakika akipata nafasi ya kucchaguliwa atakisaidia chama
kuhakikisha kinaingiza wanachama wengi zaidi.
BW.KULIGWA amewataka wagombea wenzake kufanya kampeni
za kistaarabu ili kuwezesha kufanyika siasa za ukweli na sio bora siasa kama
inavyoonyeshwa na baadhi ya wapambe wa wa baadhi ya wagombea ambao wamejitokeza
kumchafua.
END.
Comments
Post a Comment