USAFI WAZUA MTAFURUKU KIBAHA MJINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, 07 May, 2014

Mvutano mkali unaendeleakati ya uongozi wa halmashauri ya mji wa Kibaha na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kandokando ya eneo linaloitwa soko mjini Kibaha kufuatia kampeni ya usafi inayoendelea.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia wananchi wenye hasira wakijaribu kuzuia utekelezaji wa kampeni hiyo ya usafi, ambayo ilikuwa inafanywa na mgambo wa halmashauri wa mji wa Kibaha kwa usimamizi wa afisa ya afya Kata Mailimoja, BW.ABUBAKAR SHAH ambaye amesema suala la usafi ni jambop la lazima na kila mmoja wetu anapaswa kuwajibika katika eneo lake.

BW.SHAH ameongeza kuwa halmashauri ya mji wa Kibaha ina utaratibu wake ambao imejiwekea kwa kuzingatia sheria ndogo ndogo zinazohusiana na usafi wa mazingira ya mji wa Kibaha, ambapo imepigwa marufuku kwa mtu yoyote kutupa taka ovyo, ambapo ukikamatwa unatozwa faini ya shilingi 50,000/-

Afisa huyo wa afya Kata ya Mailimoja amefafanua kutokana na utaratibu huo, ndio maana kampeni ya usafi inaendelea katika mji mzima wa Kibaha, pamoja na kuwepo kwa wananchi wanaojaribu kupotosha zoezi hilo kwa kuzuia utekelezaji wake.

Naye mfanyabiashara ndogondogo ya kukaanga mihogo,Bibi Ashura Juma amelalamikia hatua hiyo ya halmashauri ya kuvunja Kibanda chake cha biashara ambayo alikuwa anaitegemea kuendeshea maisha ya kila siku.

Bi.ASHURA ameitaka halmashauri ya mji kuwa na huruma wakati wa utekelezaji wa operesheni za usafi ili kuepusha hasara zisizo na lazima na hasa ikizingatiwa hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi walio wengi, ambao wengi wao wameamua kujiunga na sekta isiyo rasmi kujikwamua.

Naye KACHINGWE KASERENGE ameitaka halmashauri kutoa taarifa mapema kwa wananchi kabla ya kutekeleza kampeni ya usafi wa mazingira ambayo mara nyingi uambatana na uharibifu wa mali na umwagaji wa vyakula ili kuepusha hasara kwa wajasiriamali wadogo, ambao hadi sasa hawanajatengewa eneo maalum ya kufanya shughuli zao.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA