TAG YAADHIMISHA MIAKA 75 TOKA KUANZISHWA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/5/11/2014 1:34:07 PM
Kanisa la
TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, linaadhimisha miaka 75 toka kuanzishwa kwake
ulimwenguni, kwa kufanya shughuli mbalimbali za kitumea kuelekea kilele chake
kitakachofanyika mkoani Mbeya.
Mchungaji HEBRON
KAYANGE wa Kanisa la TAG kwa mfipa Mjini Kibaha amesema kuwa kanisa lao
limeanzishwa mwaka 1939 na mpaka 2014 kanisa hilo linatimiza miaka 75,
Mchungaji
KAYANGE kwa kibaha Kanisa la TAG Kibaha
kwa Mfipa limeanzishwa Mwaka 1999 likiwa na waumini wane, lakini mpaka sasa
kanisa hilo limekuwa linakua kwa kasi kutokana na kutilia mkazo suala la mavuno
ya watu kwa kuwapatia mafundisho mbalimbali ya kiroho.
Mchungaji
KAYANGE amebainisha kuwa kanisa lake limekuwa linatoa huduma mbalimbali za
kijamii ikiwa pamoja na kushirikiana na jamii inayowazunguka katika masuala ya
kusaidia watoto yatima,kubadilisha tabia ya vijana ambao wanatumia madawa ya
kulevya, ili kuwa raia wema.
Na kwa
kuliona hilo Kanisa la TAG Kwa mfipa waliandaa chakula cha mchana ambacho
walikula kwa pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya ambao walijitokeza kwa
wingi kuunga mkono hatua za kanisa hilo kuwabadilisha kitabia.
Naye mwenyekiti
wa serikali ya Mtaa wa Kwa mfipa, BW.HAI MSHAM HAI amelipongeza kanisa hilo kwa
kuweza kushirikiana na serikali katika kurekebisha maadili yanayomon yoka kwa
kasi katika jamii.
BW.MSHAM
amebainisha kuwa ni wajibu wa viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika
kupambana na mmonyoko wa maadili kunakoshika kasi siku hadi siku na kutishia
kuwa na Taifa lisilo na nidhamu na kukosa utiifu kwa vizazi vijavyo, kama hatua
za haraka hazijachukuliwa kupambana na hali hiyo.
END
Comments
Post a Comment