AJALI MWISHONI MWA MWAKA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/31/2013 10:39:12 AM Pamoja na jitihada mbalimbal;I zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kupunguza ajali zisizo na lazima, baadhi ya madereva wameonyesha kupuuza kwa tahadhari hizo na kusababisha ajali ambazo zinawasababishia vifo au ulemavu. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia ajali iliyosababishwa na mwendo wa kasi baada ya gari ndogo aina ya TOYOTA iliyokuwa inasafiri kati ya Bagamoyo na Mlandizi kuacha njia na kuvamia vibanda vya wafanyabiashara. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mbwawa, BW.RAMADHAN KONDO amebainisha kuwa gari hiyo iliacha njia na kugonga vibanda vya wafanyabiashara, na aliyejeruhiwa ni mtu mmoja, BW.JAFFAR YOHANA ambaye alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi. BW.KONDO amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. END.