WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/01/07/2017 11:19:32
Wananchi nchini
wametakiwa kutoa ushirikiano katika kusaidia juhudi za serikali katika
mapambano dhidi ya rushwa ili kuleta
matokeo yanayotarajiwakatika vita hivyo.
Mwezeshaji katika
jukwaa la ufahamu la kiraia la kila mwisho wa mwezi linaloandaliwa na asasi ya kiraia ya YOUTH
PARTNERSHIP COUNTRYWIDE-YPC-, BW.ISRAEL ILUNDE amesema ili mapambano hayo
yafanikiwe wananchi hawana budi kutoa ushirikiano wa hali na mali ili
kufanikisha malengo hayo.
BW.ILUNDE
amesema kuwa nafasi ya umma katika
mapambano hayo ni kubwa kwa wenyewe kuwa utayari katika kutokubali
kuyakaribisha wao binafsi katika ushiriki wa vitendo vya upokeaji na utoaji
rushwa ili kuziba mianya ya inayosababisha uwepo wa rushwa nchini.
Akitoa mfano
wan chi ya Rwanda kupitia taasisi yao ya kupambana na rushwa OMBUDSMAN ambayo
imekuwa ikishirikisha watu makundi yote ya kijamii katika kuwaunganisha bila
kujali nafasi zao katika jamii.
Mshiriki katika
jukwaa hilo, BW.SUBIRA JUMA amesema wao
kama vijana wana wajibu wa kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana
na umuhimu wake katika maendeleo ya nchi na kutaka kuiga nchi ya Rwanda kwa
kushirikisha makundi yote katika jamii.
Jukwaa la
ufahamu wa kiraia linafanyika kila siku ya ijumaa ya mwisho wa mwezi na
kuandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP
COUNTRYWIDE-YPC- lenye maskani yake mjini Kibaha na kufadhiliwa na Taasisi ya
FREDRICH EBERT STIFTUNG ili kuwajengea wananchi kuwa na ufahamu na harakati
mbalimbali zinazofanyika katika utekelezaji masuala ya kimaendeleo.
END
Comments
Post a Comment