WAFANYABIASHARA SOKO LA JIONI MAILIMOJA WAOMBA HURUMA YA RC NDIKILO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/06/07/2017 14:08:59
Mkuu wa mkoa
wa Pwani Mhandis EVARIST NDIKILO amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara
nyakati za jioni pembeni mwa barabara kuu ya Morogoro kuondoka ili kuwezesha
kupendezesha sura ya mji wa Kibaha.
Akiongea na
wananchi hao katika kituo cha mabasi ya Mikoani, Kibaha Maili moja, MHANDISI
NDIKILO amesema wanatakiwa kuondoka eneo
hilo ili kuwezesha kupandwa kwa majani ili kuleta sura nzuri ya Mji wa Kibaha.
Hivyo
amemwagiza Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Pwani Mrakibu msaidizi
ABDI ISSANGO kuhakikisha kuwa mabasi yote ya abiria lazima yanapita katika soko
lililojengwa hivi karibuni LOLIONDO kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara
hao kufaidika.
Kwa upande
wa wafanyabiashara wenyewe wameshindwa kuelewa dhana hiyo na baadhi yao akiwamo
BI. STELLA PETER amesema kuwa wao wenyewe ndio wanaofanya biashara katika Soko
la Loliondo na wanahamia eneo hilo la barabarani muda wa soko unapoisha saa
kumi na mbili jioni, kutokana na kutokuwepo kwa umeme katika soko jipya.
Naye
mfanyabiashara BI.NURU SAGIRE ametoa sababu ya wao kufanya biashara pembezoni
mwa barabara kuu ya Morogoro ni kutokana na kuwapo kwa wahitaji wengi wa huduma
wanazotoa kulinganisha na Soko la Loliondo na wanatumia takriban masaa manne tu
eneo hilo na kuhamisha meza zao bila kuwapo kwa uharibifu wowote wa mazingira.
INSERTS-NURU
SAGIRE, STELLA PETER, ROSE JOHN, MRS.K
INSERTS
2-RTO-ABDI ISSANGO NA RC-EVARIST NDIKILO
END
Comments
Post a Comment