VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA NIDHAMU KITUO CHA MABASI MLANDIZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/04/07/2017 13:33:28
Katika kuhakikisha
kunakuwepo na amani na usalama katika kituo cha mabasi cha Mlandizi chama cha
madereva na makondakta wa mabasi ya abiria ya Dar-es-Saalam kuelekea maeneo ya
Mkoa wa Pwani wamechagua viongozi ambao watakuwa na jukumu la kusimamia nidhamu
katika kituo hicho.
Uchaguzi hiyo
umefikiwa baada ya Diwani wa Kata ya Janga BW. CHANDE MWALIKA kupokea
malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi ambayo yanayohusiana na kero
zinazosababishwa na wapiga debe wanaofanyakazi kiholela katika eneo hilo.
BW.MWALIKA
amesema kuwa kwa kuliona hilo amechukua hatua hiyo ya kuwaita makondakta na ili
kupata mwafaka juu ya kupunguza wimbi la vijana wa kihuni ambao wamejiunga
kiholela na kazi ya kupiga debe na hivyo kuwadhalilisha abiria hususan wa kike
wanapofika eneo hilo kwa ajili ya huduma ya usafiri.
Viongozi waliochaguliwa
katika kipindi cha mpito ni Mwenyekiti BW. RICHARD MILINGA na Makamu mwenyekiti
ni BW. BARNABAS JAKA, Katibu BW. BAKARI
JUMANNE na Katibu msaidizi BW.HAMIS CHENJETU na Mweka hazina BW. KESSY KOMBO na
wajumbe wengine sita.
Katibu wa
chama cha wafanyakazi wa vyombo vya usafirishaji (TAROTWU}, BW.SALUM ABDALLAH amewataka
viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanafuata taratibu zilizopo kukiendesha
chama hicho bila kusababisha manung’uniko kutoka kwa wanachama wao.
Na ameawasititiza
kuangalia uwezekano wa kuhakiki upya
watu wanaofanya shughuli katika kituo cha mabasi Mlandizi ili kuepusha
kutoa mwanya kwa wahalifu kujipenyeza na kufanya vitendo vina vyowadhalilisha
abiria.
END
Comments
Post a Comment