POLISI RUKWA LAWAMANI KUZEMBEA KESI YA MAUAJI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12/06/2017 11:35:07
Katika hali
inayoashiria kuwa bado baadhi ya watumishi wa Jeshi la Polisi kushindwa kwenda
na kasi ya utendaji ya serikali ya awamu ya tano, Polisi katika halmashauri ya
wilaya ya Sumbawanga wamewaachia huru katika mazingira ya kutatanisha
wamewaachia huru watuhumiwa wa mauaji na wao kuendelea na vitisho.
Watuhumiwa hao
BW.YEGELA SHIGELA na BW.DOTTO PETER ambao awali walimtishia Diwani wa Kata ya
Kipeta, BW RASHID DAUD KALELE na hatimaye kufanikiwa kumuua mke wake, BIBI
MONICA MASIGANI kwa kumkata na shoka kichwani na kusababisha kifo chake.
Tukio hilo limetokea
licha ya Diwani huyo kutoa taarifa ya kituo cha Polisi Kata ya Kipeta na kukosa
msaada na hata yalipotokea mauaji, Polisi hao waliwaachia huru watuhumiwa na
wao kuendelea kutoa vitisho ambapo walimpigia simu saa saba usiku na kumuambia
kwamba amewashtaki na wao sasa wapo huru hawatishi kwa lolote.
Diwani huyo BW.
RASHID DAUD KALELE ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Baraza la madiwani
halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kutokana na tukio hilo amelazimika kukimbia
makazi yake kuepuka kuuwawa na watu hao kutokana na Polisi kushindwa kuwapeleka
mahakamani, amemuomba Waziri wa mambo ya ndani na IGP kumsaidia na kadhia hiyo
inayomkabili.
Mwandishiwa habari
hizi alipompigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna msaidizi wa
Jeshi la Polisi GEORGE SIMBA KYANDO amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kweli watuhumiwa wameachiwa huru kufuatia Mwanasheria wa serikali kudai kuwa
hakuna ushahidi wa kutosha juu ya watu hao.END
END
Comments
Post a Comment