MLIPUKO WA UGONJWA WA NGURUWE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/13/06/2017 12:59:37
Halmashauri ya
mji wa Kibaha imepiga marufuku usafirishaji na uuzaji wa nguruwe kutokana na
mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe uliotokea katika mji wa Kibaha.
Afisa
habari, mawasiliano na uhusiano wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.INNOCENT
BYARUGABA amesema kumekuwepo na vifo vingi vya nguruwe kati ya kipindi cha
mwezi Mei katika kata za Viziwaziwa na Picha ya Ndege ambapo mpaka sasa nguruwe
71 wameshakufa.
Na timu ya
wataalamu kutoka idara ya mifugo na uvuvi walipofanya uchunguzi wa awali kubaini
sababu ya vifo vya wanyama hao kwa
mwonekano na kwa uchunguzi wa wanyama hao waliokufa zilionyesha kuwepo kwa
viashiria vya ugonjwa wa homa ya
nguruwe (African swine fever}.
INSERT
Daktari wa
mifugo wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. DEOGRATIUS MGUTE amesema wao kwa
upande wao wanaendeleakupita maeneo mbalimbali ya mitaa na kata zote ili kutoa
elimu na kusimamia udhibiti wa ueneaji wa ugonjwa huo.
END
Comments
Post a Comment