UHURU WA HABARI HATARINI,
Ben Komba-
Katibu Chama Cha Waandishi Habari,Pwani
Hatua ya
Rais Magufuli kuleta mabadiliko ya kijamii kwa Watanzania kwa sasa inaonyesha
kuna baadhi ya watu wanapotosha dhana nzima ya kwa kuiga aina ya utendaji kazi
ambayo sio asili yao na matokeo yake kuna wananchi maskini ambao ndio
waliolengwa kusaidiwa na juhudi za Rais kuwaondolea adha ndio wanaoumizwa na
waigizaji.
Tunashuhudia
baadhi ya Mawaziri wa awamu ya tano wakipita huko na huko kuwajengea wananchi
hofu kwa kutoa kauli ambazo zenyewe tu zinaonekana hazijaenda shule, kwa ajili
tu labda kupitia mchakato wa kidemokrasia kandamizi wamebahatika kugawiwa vyeo
ambavyo hawastahili.
Kwanza nikianzia
suala la bomoabomoa ambalo wenyewe wanadai limelenga kuhakikisha maeneo ya wazi
ambayo yamevamiwa na kujengwa nyumba kinyume cha taratibu linafanyika bila
kufuata taratibu za kiutu na kuwasababishia wananchi umaskini zaidi, kutokana
na baadhi ya watendaji kuingiza masuala binafsi wakati wa utekelezaji wa zoezi
hilo.
Binafsi nimeshangazwa
sana na utaratibu uliotumika wa kuvunja soko ambalo jamii ya Picha ya ndege
mjini Kibaha ilikuwa inalitegemea kupata huduma muhimu ya bidhaa mbalimbali,
bila halmashauri kujenga soko jingine, hatua kama hizo hazimsaidii mwananchi wa
kawaida ambaye hana uhakika wa kipato na badala yake imekuwa hukumu kwao.
Wananchi siku
zote wamekuwa wahanga wa maamuzi ya viongozi ambao wanajidai wanawatakia mema
ilihali wanawakandamiza na kurudisha nyuma maendeleo yao, Mpaka sasa wananchi
kibao wameshaathirika na hatua kandamizi zinazofanywa na mawaziri
wanaolazimisha umaarufu wa haraka haraka.
Basi ni lini mwananchi wa kawaida atafaidika na
uhuru wa nchi yake, Ingawa kuna hatua mbalimbali ambazo serikali ya awamu ya
tano imezitekeleza ambazo zinaathari chanya moja kwa moja kwa mwananchi wa
kawaida na kwa Taifa katika suala zima la kukuza uchumi wa Taifa ambalo ni
upunguzaji wa tozo mbalimbali za umeme.
Lakini cha
kusikitisha pamoja na upendeleo huo kwa
wananchi kuna tatizo kuhusiana na serikali ya awamu ya tano inavyoshirikiana na sekta isiyo rasmi katika
utoaji wa ajira kwa kuibua vikwazo mbalimbali ambavyo havina mashiko.
Mfano mzuri
ni katika upande wa habari, ambayo watendaji wake wanakuambia ni kazi ya wito
ambayo huwezi kuifananisha na udaktari wa uhandisi kitaaluma, ambapo kuna
taarifa ya kutaka waandishi wote lazima wawe na digrii ili kuweza kufanya kazi
hiyo.
Hatua hiyo
inachukuliwa ni kama hatua ya makusudi ya kuhujumu uhuru wa habari ili kutoa
fursa kwa siri mbaya za mafisadi wanaoila nchi hii kama walavyo mkate na
kuwacheka pamoja na kuwahujumu wanaonyonywa na kuonewa kwa kutumia vyombo vya
dola na sheria kandamizi ambazo hazina nia njema na maisha ya Watanzania walio
wengi.
Inashangaza Waziri
anatumia fedha za serikali kwa ajili ya kufanya ziara ya kutangaza vita dhidi
ya vyombo vya habari bila kujali taratibu za kitaaluma kwa kulazimisha
waandishi wote wawe na digrii, hali
ambayo huwezi kuikuta katika maeneo mengine yaani hospitali na serikalini
kwenyewe kwenye utaratibu kama huo.
Tena sehemu
zenyewe muhimu kwa maisha ya wanadamu, Lakini kwa waandishi lazima wawe na
digrii wote, kwa upande wangu mimi naona hatua hiyo imekaa kisiasa zaidi kuliko
kitaaluma ambapo kuna watumishi wa viwango tofauti vya kielimu katika upande wa
sekta ambayo siyo rasmi ya habari, kulazimisha waandishi wote wawe na digrii
bila kuwasaidia kuipata hiyo digrii huo ni udikteta ambao ushaanza kuota mizizi
na kuathiri wananchi maskini walio wengi.
Ni vizuri
watu wa kawaida wasichukuliwe kama mbuzi wa kafara, kwa ajili ya watu kujikweza
juu yao ili waonekane wanachapakazi kwa kuharibu maisha ya walio wengi na huko
ni kukiuka haki za binadamu mchana kweupe.
Huwezi kuwalazimisha
waandishi wa habari wawe na digrii wakati kuna watendaji kibao ambao
wanasemekana wana vyeti vya kufoji, tatizo ambalo ni kubwa sana upande huo,
kiasi hata cha kuhatarisha ajira ya kipindi alipokuwa NECTA, Waziri Ndalichako
kwa waliofoji kumfanyia vurugu alipotaka kufanya uhakiki wa vyeti vya wakubwa
mbalimbali ambao wanamiliki vyeti vya kufoji.
Na tulishuhudia
maandamano na upinzani kutoka kwa vigogo ambao wanasemekana kughushi vyeti na
kuliletea Taifa hasara kutokana na kuwepo katika nafasi ambazo hawawezi
kuzitumikia ipasavyo.
Mpaka sasa
serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuongeza wimbi la wasio na ajira kutokana
maamuzi ya kujionyesha yanayofanywa na baadhi ya mawaziri ambao kiuhalisia ni
wapigaji tu na sio makini na ambao wengine wamepata nafasi hizo kwa kupora
ushindi wa waliostahili na kujivisha wenyewe kwa kutumia nguvu kubwa za dola
ambazo chama tawala inazo.
Ili suala la
kuweka digrii mbele kuliko akili ya kawaida (common sense) ambayo inatolewa
kama karama kwa baadhi ya wanadamu, Linatakiwa kupingwa kwa nguvu zote na ndio
maana vidole vya mkono havifanani, hatuwezi wote kuwa na digrii ikiwa nchi
haina hata mtaala wa uandishi wa habari ambao mi binafsi ninao kutoka Uingereza
ambao WRITERS BUREAU walinipatia na kujisomea nyumbani ili niweze kupata
mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yangu ya kila siku, Kuleta makuzi katika
masuala muhimu ya Kitaifa kutaathiri kwa njia moja au nyingine maendeleo ya mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kufanya maamuzi
ya kukomoana hakutasaidia chochote badala yake kutaathiri juhudi ya serikali
kuwaletea wananchi maendeleo yao na toka wanahabari wamekuwa wanafanya kazi kwa
karibu na taasisi nyeti za serikali na kuheshimka maeneo hayo.
END
Comments
Post a Comment