PCCB PWANI YATOA RIPOTI YA ROBO YA KWANZA 2016
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/13/04/2016 15:52:46
Ofisi ya
TAKUKURU (M) Pwani katika kipindi cha robi ya kwanza ya mwaka 2016 imefanikiwa
kutekeleza majukumu yake katika kuielimisha jamii na kufanya uchunguzi wa
tuhumaa mbalimbali zinazohusiana na rushwa.
Kamanda wa
TAKUKURU mkoa wa Pwani, BI. SUZAN RAYMOND amezungumza hayo wakati wa kikao na
waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo mjini Kibaha, amesema katika
mkipindi hicho taasisi hiyo imefanya uchunguzi na uchambuzi wa mifumo kwa lengo
la kubaini mianya ya rushwa na kutoa ushauri wa namna ya kuiziba katika
taasisoi na idara mbalimbali.
BI.SUZAN
ameongeza kwamba katika kipindi hicho ofisi yake imepokea malalamiko 64 kati ya
hayo 49 yanahusiana na vitendo bvya rushwa na uchunguzi wake unaendelea na
malalamiko 15 hayakuhusiana na vitendo vya rushwa ambapo walalamikaji walishauriwa kupeleka kero zao katika idara
husika.
Kamanda huyo
wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani BI SUZAN RAYMOND ametaja kama serikali za mitaa ndio
kinara wa rushwa na wilaya ambayo imeathirika zaidi ni Bagamoyo.
END.
Comments
Post a Comment