LICHA KUPEWA KIPAUMBELE WAGONJWA WA UKIMWI WAKOSA HUDUMA MUHIMU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/20/04/2016 13:06:37
Imegundulika
mjini Kibaha kuwa mradi wa kuwasaidia wagonjwa walio majumbani ambao ulikuwa
unasimamiwa na chama cha msalaba mwekundu Tanzania umeshindwa kukidhi mahitaji
ya wagonjwa ambao walikuwa wanalengwa.
Kwa mujibu
wa watoa huduma majumbani ambao mwandishi wa habari hizi amefanikiwa kuongea
nao, Mmoja wao BW. RAJAB NGONJI ameeleza yeye amekuwa akifanya kazi hiyo kwa takriban
miaka kumi lakini anachokiona sasa ni tofauti sana na awali.
Bw.
NGONJI amesema mradi huo unaofadhiliwa
EGPAF na PATHFINDER na kusimamiwa na Chama cha Msalaba mwekundu umekuwa
ukiendeshwa kwa kuangalia zaidi gharama za uendeshaji wa Ofisi na kujilipa
mishahara na posho na kuwaacha wagonjwa wanaangamia majumbani kwa kukosa madawa
na lishe.
BW. NGONJI
ameongeza kuwa hapo awali wagonjwa walikuwa wanapatiwa misaada mbalimbali
ikiwamo na madawa, kitu ambacho sasa hakuna na hivyo kuwafanya wagonjwa
kunufaika kidogo na msaada unaotolewa kwao.
Naye BW. MICHAEL BEDA mhudumu wa afya kutoka mtaa
wa Kibondeni amesema kumekuwepo na usumbufu mkubwa linapokuja suala la kulipwa
posho ambazo Shirika la Msalaba Mwekundu wanatumia M PESA kuwalipa na hivyo
kusababisha usumbufu mkubwa.
BW. BEDA
amefafanua kuwa wamekuwa wakisubiri mpaka miezi mitatu bila kulipwa posho na hivyo kufanya zoezi la
kutembelea wagonjwa kuwa gumu na hasa pale wagonjwa wanapohitaji misaada
midogomidogo kama fedha za sabuni, chakula na madawa.
Naye mratibu
wa mpango huo wa kuhudumia wagonjwa majumbani wilayani Kibaha BI. AGNES LIBOGA amejibu
madai hayo kwa kudai kuwa wao hawahusiki na utoaji wa chakula kwa wagonjwa
ambao wamesendeka, kuhusiana na suala kucheleweshwa kwa posho kwa watoa huduma
majumbani amebainisha kuwa wameshaanza kulipwa posho zao za miezi mitatu.
END
Comments
Post a Comment