WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09:54/22/2/2014 Serikali ya Mtaa wa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kushirikiana na wananchi imeamua kujenga daraja kwa njia ya kujitolea ili kupunguza kero wanazopata kipindi cha msimu wa mvua. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWICHE amesema wameamua kuchukua uamuzi kutokana na kero zinazowakabili kipindi cha mvua na kusababisha maisha ya wananchi kuwa hatarini. BW.LINGOWICHE ameongeza kuwa kinachosaidia katika ujenzi huo wa makaravati ni kutokana na wananchi wake kuwa wenye kuzingatia mambo na kumuelewa pale alipoitisha kikao cha wananchi kuwaelezea kusudio la wananchi kujitolea kujenga makaravati hayo. Amefafanua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha, BW.SYLVESTER KOKA ametoa shilingi laki sita na wananchi wakichangia shilingi laki 2, na kuwezesha kuchongwa kwa barabara hiyo inayounganisha mtaa huo. \Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara Mtaa wa Muheza, BW. ASHRAF MMARI amesema mpaka sasa ujenzi wa ...