Posts

Showing posts from September, 2012

MAMA WA KAMBO ATESA MWANA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-09-30/09:21:22 Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mlandizi, BI. MIRIAM MBWANA amemuhukumu muuguzi BI. JOSEPHINE CHARLES wa kituo cha afya Mlandizi kilichopo katika wilaya ya Kibaha, kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili na fidia ya shilingi 150,000/= kwa ajili ya kumtesa mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 6. Akitoa hukumu hiyo HAKIMU MBWANA amesema kufuatia uwepo sheria ya haki ya mtoto ambayo inasisitiza katika kumlinda na kumpatia haki stahili mtoto na si vinginevyo, kutokana na hilo hakimu huyo ameamuru mtoto huyo ambaye jina limehifadhiwa akabidhiwe kwa Afisa ustawi wa jamii BW. SAID MBEGU mpaka hapo mama yake mzazi atakapopatikana. Hali hiyo inafuatia wakazi wa mtaa wa Kaloleni uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi kuungana kunusuru maisha ya mtoto wa kambo, Ambaye mumewe BW. CHARLES JULIUS DINDA amezaa na mama mwingine, na yeye kumpata BI. JOSEPHINE CHARLES ambaye amezaa naye mtoto mmoja ambaye ana...

DSTV WITH RELIGIOUS DISCRIMINATION

Michael Ajewole 2:18am Sep 16 RE: REMOVAL OF EWTN FROM THE DSTV NETWORK The news is no longer new that EWTN, the darling channel of most Catholics worldwide, particularly in Nigeria, has been yanked off the satellite DSTV network since about a week. From my investigations and contact with the African representative of EWTN, the reasons given are that the channel is non-performing meaning practically that not enough people in Nigeria are watching it. This of course cannot be true because: a. We of the communications apostolate have been inundated with protests messages since it was yanked off and same goes for the EWTN African representative and others internationally. b. No other religious channel has been so treated and we do not believe at all that we are the least of all channel captive audiences off all religious networks. Even of others go, the only Catholic 24 hour satellite channel known amidst the cacophony of religion channels in Africa must not be allowed to go. EWTN h...

TTCL PWANI YAIBIWA NYAYA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/19/12/18:56:24 Shirika la simu katika Mkoa wa Pwani -- TTCL-- limekumbwa na wimbi la kuibiwa nyaya za kusambazia miundombinu ya simu katika Maeneo ya mamlaka ya mji wa Kibaha na wilayani Kisarawe na hivyo kuathiri utoaji wa huduma hiyo ya mawasiliano kwa simu za waya. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Kibaha, Meneja wa TTCL mkoa wa Pwani, BW. FRANCIS MWENDA amesema kuwa wizi huo uetokea maeneo ya TAMCO kati ya Agosti 11 mwaka huu majira ya saa 1.30 na saa 2.00 na kuathiri wateja takriban 30. BW. MWENDA ameongeza waya ulioibiwa ulikuwa na urefu wa mita 180, ambapo mtuhumiwa amekamatwa japo anajifanya hamnazo anapotakiwa kujitambulisha kwa kutaja majina tofauti kila wakati, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa. Aidha BW. MWENDA amefafanua kwamba matukio hayo ya wizi yamekuwa yanashika kasi kiasi cha kusababisha wilaya ya Kisarawe kukosa mawasiliano kw karibu wiki mbili sasa kutokana na hujuma ambayo...

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI BARABARA-MSATA - BAGAMOYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/09/18/2012/18:37:04 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JAKAYA KIKWETE amewataka madereva kuwa makini wanapoendesha magari yao ili kuepusha vifo na majeruhi, ambapo katika kipindi cha mwaka 2011 watu 3100 walikufa katika ajali za barabara na kati yao wengine zaidi ya elfu 22 walijeruhiwa katika ajali hizo. DKT. KIKWETE ameongea hayo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Msata- Makofia-Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 64, ambapo amesisitiza kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kutopotosha nia ya serikali kueneza mtandao wa barabara zenye kiwango cha lami nchi nzima. DKT. KIKWETE amefafanua kuwa barabara hiyo itafungua fursa ya maendeleo kwa wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake hasa kwa kuzingatia kuwa itakuwa ni kichocheo cha maendeleo hususan kwa wakulima wa kilimo cha mananasi wa Kiwangwa ambao kutokana na ubovu wa barabara uliokuwepo m,ananasi yao yalikuwa yanaozea mashambani wakati wa kipindi cha mvua. Aidha amewaasa wa...

MJI WA KIBAHA KUFAIDIKA NA USHIRIKIANO

Ben Komba/Pwani- Tanzania/9/17/12/19:00:02 Ushirikiano uliopo kati ya halmashauri ya mji wa Kibaha na manispaa ya manispaa ya mkoa wa kisiwa cha GOTLAND, utainufaisha kwa kiasi kkubwa katika suala la demokrasia na, usambazaji wa maji safi na salama, utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisisni kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. ABUDADI MKOMAMBO amesema uhusiano huo kati ya miji hii miwili una takribani miaka 12 sasa. Ambapo BW. MKOBAMBO amebainisha katika kipindi cha miaka miwili ijayo yaani m,waka 2012 mpaka 2014, uhusiano wao umetoa kipaumbele kwa miradi kadhaa ambayo itafadhiliwa na ICLD (international center for loca demokrasi) ambayo ina lengo la kuimarisha demokrasia kwa watu wa kada ya kawaida, ikiwa pia ndio kipaumbele cha shirika la kimataifa la maendeleo la SWEDEN-SIDA- Akizungumzia suala la kuimarisha mfumo wa maji halmashauri ya mji wa Kibaha itaanzisha mirad...

WAANDISHI PWANI WASHUTUMU AMUAJI YA MWENZAO.

WAANDISHI WASHUTUMU POLISI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/09/2012 Waandishi mkoa wa Pwani wamelaani hatua ya Jeshi la Polisi kumuua kwa makusudi mwandishi mwenzao, MAREHEMU DAUD MWANGOSI wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi. ... Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Pwani, BW. JOHN GAGARIN amesema kama inavyoonekana katika Picha ambayo waandishi wa habari wanaamini inaongea maneno 1000, ndivyo tunavyofundishwa darasani, inayoonyesha askari akimlenga BW. DAUD MWANGOSI waziwazi. BW. GAGARIN ameshangazwa na hatua ya Jeshi la Polisi kuunda tume ya kuchunguza mauaji hayo, kwani ni upotevu wa fedha za umma bure, kinachotakiwa ni kuwajibika kwa viongozi wa Jeshi hilo, kwa kuanzia na yule aliyempiga risasi kwa makusudi. Wakizungumza katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Mmoja wa waandishi ambaye nimeongea naye, BW. OMARY MNGINDO amesema hatua hiyo ni mbinu za makusudi za Jeshi la Polisi kutaka kuwatisha waandishi wasifanye kazi yao kwa weledi na kuwafanya wananchi was...

BAVICHA WATAKA IGP MWEMA AACHIE NGAZI.

BAVICHA WATAKA IGP MWEMA AACHIE NGAZI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/09/03/14:56:56 Baraza la vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA-BAVICHA mkoa wa Pwani, limemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kujiuzulu nafasi ambayo anayo kutokana na Jeshi hilo kushindwa kulinda wananchi na mali zao na kujihusisha zaidi na masuala ya kuua wananchi wasio na hatia kwa msukumo wa kisiasa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA, BW. ELLISON KINYAHA amesema kumekuwepo na ongezeko la mauaji ya wananchi kila panapofanyika mikutano ya chama chao kwa lengo la kuwatisha wananchi, na ameelezea tukio la hivi karibuni kabisa la kuuliwa kwa mwandishi wa habarai wa Televisheni ya CHANNEL 10, BW. DAUD MWANGOSI kuwa ni ushahidi wa kushindwa kwa Jeshi hilo. BW. KINYAHA amebainisha kitendo hicho ni kielelezo tosha cha jinsi gani Jeshi la Polisi halizingatii haki za binadamu, kwa ajili kuwafurahisha wanasiasa wa chama tawala, ambao wameonesha kustushwa ...