Posts

TUME YATAKIWA KUHARAKISHA UCHUNGUZI

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania Chama cha ushirika wa umwagiliaji Bonde la Mto Ruvu mkoa wa Pwani wilayani Bagamoyo wameitaka tume ya uchunguzi iliyoundwa na naibu waziri wa kilimo na chakula kufanya uchunguzi huo kwa haraka ili kuweza kupata kiasi halisi cha fedha zilizopotea. Maombi hayo yametolewa kwa Mwakilishi kutoka wizara ya Kilimo na Chakula, BW.HUMPHREY NAMASITE alipokutana na wakulima wa ushirika huo, kujua hatima ya mgogoro unaoendelea katika ushirika huo. Ambapo Mwanachama wa ushirika huo SADALLA IDD CHACHA amemuomba mwakilishi NAMASITE kutoka wizarani kuwaletea matokeo ya tume hiyo iliyoundwa na Waziri badala ya kuanza kuhoji upya wanachama, kwa kufanya hivyo hatua madhubuti zinachelewa kuchukuliwa. BW.HUMPHREY NAMASITE kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula amewaeleza wanachama wa ushirika huo kuwa wao kama tume iliyoundwa kuchunguza upotevu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Bodi iliyovunjwa na Waziri ZAMBI. Zaidi jionee mwenyewe…….. ...

WADAU WA ELIMU WALALAMIKA UBORA WA KITABU

WADAU WA ELIMU WALALAMIKA UBORA WA KITABU Ben Komba/Kibaha- Pwani/15 September 2014 Sept 16 WADAU wa elimu mkoani Pwani wamemlalamikia mchapishaji na msambazaji wa vitabu vya somo la Advance Level Biology kwa ajili ya kidato cha sita kinachochapishwa na mkazi aliyetajwa kwa jina la jina tunalo (Fred Unga) kwa madai ya kukosa sifa za kuchapisha vitini hivyo. Akizungumza na mwandishi wa habari mjini Kibaha mkoani Pwani mmoja wa wadau hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Godfrey alisema kwamba vitini hivyo vinavyochapishwa na mkazi huyo ambaye ana elimu ya kidato cha nne ni sawa na kupotosha wanafunzi wenye elimu ya kidato cha sita. Alisema kuwa wamefuatilia matoleo yanayotolewa na mkazi huyo kisha kugundua hayana ubora wa kuwawezesha wanafunzi walengwa kuweza kufaulu vema kwenye masomo yao. Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mwalimu Mkuu wa Kibiti High School Wenceleslaus Kihongosi ambaye alisema mtu huyo alisoma shuleni hapo lakini hakuwahi kufanya mtihani...

VIPOFU WAWEZESHWA KUONA-VIDEO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania Serikali nchini imetakiwa kutoa kipaumbele kwa kazi za kitabibu zinazofanywa na watafiti wa tiba asili ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yanayojitokeza na kusumbua binadamu. Mtafiti wa madawa asilia mwenye maskani yake,katika eneo la Magwila Chalinze BW.ABDALLAH MBEMBENUE amesema kuwa katika utafiti wake ambao ameufanya amebaini kwamba kuna miti dawa ambayo inaweza kufanya maajabu katika kutibu magonjwa mbalimbali. Akizunguimza na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika kwa mtafiti watiba za asili kufuatia habari za kuponywa upofu kijana BW.SHOMARI KICHWECHWE ambaye alipata upofu toka Juni mwaka huu na kumfanya kuishi maisha ya mashaka kutokana na mabadiliko hayo ya kimaumbile ambayo ameyapata. BW.MBEMBENUE ameongeza kuw tiba za asili zina nafasi kubwa ya kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania iwapo wizara ya afya ikiwa makini na kukaa karibu na watafiti wa tiba asilia, ambapo kwa upande wake kuna magonjwa kadhaa amba...

MAADHIMISHO YA WIKI YA WANAWAKE-VIDEO.

Image
Ben Komba,Pwani-Tanzania/12-9-2014/11:15 Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake nchini, Umoja wa wanawake Tanzania wilaya ya Bagamoyo umetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika kituo cha afya Chalinze mkoa wa Pwani. Msafara huo wa kinamama hao ukiongozwa na Mwenyekiti wa UWT wilayani Bagamoyo, BI.HAFSA KILINDO na Katibu wa Jumuiya hiyo wilayani Bagamoyo BI.TABU HUSSSEIN walitembelea wadi ya wazazi na nyinginezo na kuwatakiaa uponaji wa haraka. Akiongea katika mkutano wa ndani na wanachama wa UWT,Katibu wa wake wilaya ya Bagamoyo, BI.TABU HUSSEIN amewataka kinamama kuhakikisha wanaandaa mazingira mazuri kwa watoto wa kike waliomaliza darasa la saba ili waweze kuendelea na masomo ya ngazi inayofuata. BI.HUSSEIN ameongeza ni wajibu wa wanawake kuwalinda watoto wao wa kike na majaribu mbalimbali na hivyo ni vyema kuwasaidia kishauri ikiwa na kubadil;I mitazamo tuliyozoea kijamii, jambo ambalo wengine wakiambiwa wanasema wamedharauliwa i...

AJALI ZAMALIZA VIJANA-VIDEO

Image
Ben Komba/Kibaha-Pwani/12-9-2014/11:15 Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku tatizo linalosababisha mamia kama si maelfu ya vijana kupoteza maisha kunakosababishwa na madereva wazembe. Mwandishi wa habari hizi katika hali ya kusikitisha alikutana kwa ana na ajali iliyopora maisha ya kijana huyu ambaye alitambulika kwa jina moja tu, La DUCHA akiwa amepata ajali ambayo iliosababisha kupoteza maisha. Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, BW.KINYOGOLI LUSONZO amesema kijana huyo akiwa anatokea kituo cha mabasi Maili moja akiwa upande wake na kwa ghafla akaona gari linakata kona kuelekea upande mwingine wa barabara kana kwamba linamkinga anayekuja na pikipiki. Kutokana na hatua ya lile gari kukata ghafla kulisabisha pikipiki hiyo kuligonga gari kwa ubavuni na yule kijana kurushwa juu na kichwa chake kupiga lami kama unavyoshuhusidia. END.

AJALI ZA PIKIPIKI ZINAVYOMALIZA VIJANA

Ben Komba/Kibah-Pwani/12-9-2014/11:15 Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku tatizo linalosababisha mamia kama si maelfu ya vijana kupoteza maisha kunakosababishwa na madereva wazembe. Mwandishi wa habari hizi katika hali ya kusikitisha alikutana kwa ana na ajali iliyopora maisha ya kijana huyu ambaye alitambulika kwa jina moja tu, La DUCHA akiwa amepata ajali ambayo iliosababisha kupoteza maisha. Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, BW.KINYOGOLI LUSONZO amesema kijana huyo akiwa anatokea kituo cha mabasi Maili moja akiwa upande wake na kwa ghafla akaona gari linakata kona kuelekea upande mwingine wa barabara kana kwamba linamkinga anayekuja na pikipiki. Kutokana na hatua ya lile gari kukata ghafla kulisabisha pikipiki hiyo kuligonga gari kwa ubavuni na yule kijana kurushwa juu na kichwa chake kupiga lami kama unavyoshuhusidia. END.