ADHA YA MAJI KIJIJI CHA GONGO KATA YA MKANGE JIMBO LA CHALINZE WILAYA YA BAGAMOYO PWANI Na John Gagarini, Mkange WANANCHI wa Kijiji cha Gongo kata ya Mkange wilayani Bagamoyo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo huweka foleni ya kuchota maji kwenye kisima kilichopo kijijini hapo baada ya wiki mbili. Kutokana na usosefu huo wa maji wananchi hao wamekuwa wakinunua maji ya bomba ndoo ya lita 20 kati ya shilingi 1,000 na shilingi 1,500 maji ambayo huuzwa kwenye magari au pikipiki hivyo kuwafanya wajikute hawapati maendeleo kutokana na gharama kubwa kuzitumia kununulia maji. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete, kwenye kata ya Mkange mwananchi wa Kijiji hicho Hungilo Nyoka alisema kuwa maji yamewafanya washindwe kupata maendeleo. Nyoka alisema kila kaya inatakiwa ichote madumu manne ili angalau kila mmoja apate baada ya hapo maji hukatika ambapo in...
Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.
Ben Komba/Pwani=Tanzania/11:56 Umoja wa Wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na mahoteli UGEHOKI mjini Kibaha wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kuendelea kutoza kodi ambayo imefutwa kisheria. Katibu wa UGEHOKI, BW.RICHARD NGELEJA amesema hayo katika mkutano wa wanachama wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa COUNTRYSIDE,Ambapo amenukuu majadliano ya kikao cha nane cha bunge cha tarehe 22 juni 2012. BW.NGELEJA amebainisha kuwa katika kikao hicho cha bunge ambacho kilijadili kuhusu ushuru wa hotel levy ipunguzwe kutoka 20% hadi 18% au 16%,na serikali inakamilisha zoezi lakuhuisha sheria ya utalii ya mwaka 2008 iliyoanza kutumika mwezi Julai,2009. Naye Mwenyekiti wa UGEHOKI, BW.FABIAN MAJAGA amebainisha kuwa wao wana vielelezo vyote vinavyoonyesha kufutwa kwa ushuru huo wa nyumba za wageni na mahoteli ikiwa pamoja hansard ya Bunge ambayo inaeleza wazi kufutwa kwa ushuru huo. BW.MAJAGA ameongeza kuwa hatua mbali mbali wamechukua ikiwa ...
Comments
Post a Comment