WAKAZI MATIPWILI BAGAMOYO WAPINGA UBABE WA MKUU WA WILAYA

MGOGORO WAIBUKA KUFUATIA UBABE WA DC-BAGAMOYO:
Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/02/2017 13:12:36
Sakata la uwekaji wa kutumia nguvu wa mpaka kati ya kijiji cha Matipwili na hifadhi ya Mbuga ya Saadani wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, limeingia katika sura mpya kufuatia Mwenyekiti wa kijiji hicho kubainisha matumizi makubwa ya nguvu katika utekelezaji wa suala hilo kunakofanywa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ALHAJI MAJID MWANGA.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Matipwili, BW. GESANDE MWISA amesema amekuwa akipokea vitisho mbalimbali ikiwa pamoja na majaribio kadhaa ya kutaka kuchonganishwa na wananchi kutokana na msimamo wake kuhusiana na utekelezaji wa mpango huo wa kubadilisha mipaka ambao utaathiri zaidi kijiji hicho.
BW. MWISA amesema kuwa eneo la mgogoro halitakiwi kuguswa na pande zote mbili mpaka kutakapopatikana muafaka ambao utawezesha kutoa ufumbuzi wa mgogoro husika.
Amesema yeye ananshangazwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kuamua kufanya jambo hilo kwa nguvu badala ya kusubiri tume ambayo imeundwa na Waziri mkuu kufika kwa ajili ya kuhakiki mipaka hiyo.
Mmoja wa Wakazi akiongea bila kutaja jina lake amesema wanashangazwa na hatua ya mkuu huyo wa wilaya kufika kijijini hapo akiwa ameambatana na magari mawili yaliyojaa Polisi na maofisa wa TANAPA ili kuweka mipaka katika eneo hilo.
Mwananchi huyo ameongeza kuwa hatua inafanana au imepita ya enzi ya mkoloni katika suala zima la ukandamizaji wa wananchi, hivyo ameomba kama kijiji hicho kipo kinyume kisheria basi na kifutwe.
Nakutokana na hali hiyo wananchi walishindwa hata kuongea kutokana nay eye kujigamba kuwa ni askari magereza na anachotaka kifanyike ndicho kitakachofanyika na suala mpaka utakuwa wapi amewaambia wananchi watulie hata kama mpaka ukiwa milangoni mwao.
Naye makazi mwanamama ameelezea kukwaza na hatua za Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kutumia mabavu kutaka kugawa eneo la kijiji hicho kwa kutumia nguvu kubwa kiasi cha kuwafanya wananchi kuichukia serikali yao.
Ameongeza kuwa wananchi waligomea kulazimishwa kuambataana na mkuu huyo wa wilaya kwenda kwenye mipaka ilihali wakijua kwamba eneo hilo lina mgogoro na haitakiwi upande wowote kujihusisha na eneo hilo.
Na tatizo hilo sio jipya kwani ni mapokeo kutoka kwa aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, BW.MAGESA MULONGO ambaye kwa njia moja au nyingine aliita pande zote mbili na kuwasuluhisha na mgogoro huo kumalizika, lakini cha kushangaza kuona mkuu wa wilaya huyu amerudisha nyuma mafanikio ambayo yalifikiwa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ALHAJI MAJID MWANGA alipotakiwa kuthibitisha juu ya tuhuma hizo, amesema kuwa yeye hana cha kujibu na kama kuna maswali yoyote basi waulizwe TANAPA na yeye hausiki ilihali yeye ndiye ambaye ametoa kauli hiyo akiambatana na magari yaliyojaa askari.
Kijiji cha Matipwili kipo kilomita 9 toka hifadhi ya mbuga ya Saadan na TANAPA wanatambua uwepo wa kijiji hicho, Lakini siku za hivi karibuni kimejikuta katika mtafaruku ambao unategemea zaidi uamuzi ambao utatolewa na tume maalum iliyoundwa na Waziri mkuu kukagua mipaka kati ya hifadhi na vijiji vinavyozunguka hifadhi za Taifa.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA