KIBAFA YAFANYA UCHAGUZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/06/03/2017 11:56:39
Chama cha
soka wilaya ya Kibaha hatimaye kimepata viongozi watakaokiongoza chama hicho
kwa kipindi kijacho, kufuatia kukosa uongozi kwa takriban miaka minane.
Katika uchaguzi
huo wa KIBAFA, wamefanikiwa kupata Katibu mpya ambaye ni DAUD MHINA na
Mwenyekiti wake ni ROBERT MUNISI kwa kushirikiana na viongozi wengine ambao
wamechaguliwa katika kuhakikisha wanaendeleza mpira wa soka Kibaha.
Akiongea baada
ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya ROBERT MUNISI amewahakikishia wapiga kura kwa
pamoja watahakikisha chama hicho cha wilaya ya Kibaha kinakuwa mfano kwa vyama
vingine vya wilaya.
Akiongea
katika uchaguzi huo, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Pwani, HASSAN HASSANOL
amekitaka KIBAFA kusimamia maendeleo ya mchezo wa soka wilayani Kibaha ili
kuwezesha vilabu vya wilayani hapa kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali
ya soka.
Ikiwa na
kuzisaidia timu zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini katika kukabiliana na
changamoto zinazozikabili zinapokuwa mashindanoni katika kuzijengea ari ya
kupambana vyema katika mashindano ambayo timu zetu zinashiriki.
Kwenye
kinyang'anyiro hicho kimewezesha kupatikana kwa viongozi 7 huku nafasi za
wajumbe zikikosa waliojaza fomu kuwania nafasi hizo, Mwenyekiti amechaguliwa
Robert Munisi kura 57, Makamu Hamidu Shebuge (57) Katibu Daud Mhina (57),
Msaidizi Ivan Chenga (56), Mhazini Mohamed Mwenda (55), Mjumbe kuwakilisha Mkoa
Edward Mgogo (57) na Mwakilishi wa vilabu Japhert Mbogo (57).
matokeo hayo yalitangazwa na Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya uchaguzi ya COREFA Mwanasheria Stephen Mwakibolwa .
END.
Comments
Post a Comment