BOHARI YA MADAWA LAWAMANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/09/09/2016 19:37:11
Bohari ya
madawa nchini imelalamikiwa kwa kushindwa kukidhi mahitaji ya halmashauri
zilizopo katika Mkoa wa Pwani kutokana na dawa kuagizwa na matokeo yake kupata
madawa kiduchu.
Akizungumza katika
kikao cha Baraza la ushauri la mkoa, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Kibaha BI.TATU SELEMAN amesema wamekuwa wakiagiza dawa kama utaratibu
unavyoelekeza lakini badala ya kupata walichoagiza wanapata pungufu ya
mahitaji.
Ametoa mfano
unaweza kuagiza dawa za shilingi milioni 9 lakini wao wanakupa madawa ya
shilingi milioni 2 na hivyo kuwalazimu wahitaji kuanza zoezi la ufuatiliji
bohari ya dawa.
Awali akifungua
kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Pwani,
Mhandisi EVARIST NDIKILO amesema kuwa kupitia kikao hicho anategemea
changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi na upungufu wa madawa
zitapatiwa ufumbuzi.
END.
Comments
Post a Comment