TIBA ZA ASILI ZIPEWE KIPAUMBELE
Ben Komba/Pwani-Tanzania Serikali nchini imetakiwa kutoa kipaumbele kwa kazi za kitabibu zinazofanywa na watafiti wa tiba asili ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yanayojitokeza na kusumbua binadamu. Mtafiti wa madawa asilia mwenye maskani yake,katika eneo la Magwila Chalinze BW.ABDALLAH MBEMBENUE amesema kuwa katika utafiti wake ambao ameufanya amebaini kwamba kuna miti dawa ambayo inaweza kufanya maajabu katika kutibu magonjwa mbalimbali. Akizunguimza na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika kwa mtafiti watiba za asili kufuatia habari za kuponywa upofu kijana BW.SHOMARI KICHWECHWE ambaye alipata upofu toka Juni mwaka huu na kumfanya kuishi maisha ya mashaka kutokana na mabadiliko hayo ya kimaumbile ambayo ameyapata. BW.MBEMBENUE ameongeza kuw tiba za asili zina nafasi kubwa ya kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania iwapo wizara ya afya ikiwa makini na kukaa karibu na watafiti wa tiba asilia, ambapo kwa upande wake kuna magonjwa kadhaa ambayo hayampi shida k...