MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA-VIDEO
Ben Komba-Pwani-Tanzania-25=4-2014 Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini, maiti tano zimepatikana zikielea katika Mto Mpiji kufuatia kusombwa na maji walipokuwa wanajaribu kuvuka daraja linalounganisha kati ya wilaya ya Kinondoni na halmashauri ya mji wa Kibaha. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Lumumba, BW.GIDEON TAIRO amethibitisha kuwatambua marehemu hao ambao ni BW.JAJI MNEMWA na BW.MUSHI ambao walikuwa wanafanya shughuli zao za uzalishaji mjini Dar es Saalam na ni wakazi wa eneo lake. BW.TAIRO ameongeza kuwa kwa kupatikana kwa miili kumesababisha idadi ya waliokufa na maji katika mto Mpiji kufikia watano, wane wakiwa wanaume na mmoja mwanamke. BW.TAIRO amebainisha kuwa kwa muda mrefu wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiomba kujengwa kwa daraja la kudumu katika eneo hilo ili liweze kupitika kipindi chote cha mwaka na hasa ikizingatiwa linatumika na watu wa kada mbalimbali katika jamii, hususan wanafunzi, wazee na kinamama wajawazito. Naye Katibu w...