BABA ATELEKEZA FAMILIA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, April 11, 2012/.06:48:08 PM Mama mmoja mkazi wa mjini Kibaha BI. DIGNA LAURENT MASHAKAhivi karibuni amekumbwa na kisanga cha kutelekezewa watoto na mali za familia kuuzwa na mume wake wa ndoa, kwa sababu ya ndoa yao kuingiliwa na Mama mmoja mjane mkristo wa TAG anayejulikana kwa jina la Mama BETTY ambaye awali alikuwa anadai ana undugu na Mume wa mlalamikaji lakini kumbe ni kinyume chake. BI. DIGNA MASHAKA amebainisha mgogoro ulianza kwa yeye kuitwa mchawi na mume wake, na katika madai yake hayo siku moja mumewe BW. LAURENT MASHAKA (Michuzi) alirudi nyumbani na kumwita aende chumbani na mara alivyoingia akaanza kumkaba kiasi cha majirani kujitokeza na kuja kumuamulia, huku akidai ameweka uchawi kwenye viatu vyake na hivyo kumsababishia kupata fangasi. Na kutokana na tukio hilo BI.DIGNA MASHAKA aliamua kufungua kesi ya dhidi ya mume wake akilalamikia kitendo kilichofanywa naye, na lengo sio kuachana na mumewe, lakini kesi hiyo iliendeshwa kw...