Posts

WANAWAKE PWANI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA TANZANIA YENYE VIWANDA

Image

KIBAFA YAFANYA UCHAGUZI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/06/03/2017 11:56:39 Chama cha soka wilaya ya Kibaha hatimaye kimepata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi kijacho, kufuatia kukosa uongozi kwa takriban miaka minane. Katika uchaguzi huo wa KIBAFA, wamefanikiwa kupata Katibu mpya ambaye ni DAUD MHINA na Mwenyekiti wake ni ROBERT MUNISI kwa kushirikiana na viongozi wengine ambao wamechaguliwa katika kuhakikisha wanaendeleza mpira wa soka Kibaha. Akiongea baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya ROBERT MUNISI amewahakikishia wapiga kura kwa pamoja watahakikisha chama hicho cha wilaya ya Kibaha kinakuwa mfano kwa vyama vingine vya wilaya. Akiongea katika uchaguzi huo, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Pwani, HASSAN HASSANOL amekitaka KIBAFA kusimamia maendeleo ya mchezo wa soka wilayani Kibaha ili kuwezesha vilabu vya wilayani hapa kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya soka. Ikiwa na kuzisaidia timu zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini katika kukabiliana na changamoto zinazo...

WAKAZI MATIPWILI BAGAMOYO WAPINGA UBABE WA MKUU WA WILAYA

MGOGORO WAIBUKA KUFUATIA UBABE WA DC-BAGAMOYO: Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/02/2017 13:12:36 Sakata la uwekaji wa kutumia nguvu wa mpaka kati ya kijiji cha Matipwili na hifadhi ya Mbuga ya Saadani wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, limeingia katika sura mpya kufuatia Mwenyekiti wa kijiji hicho kubainisha matumizi makubwa ya nguvu katika utekelezaji wa suala hilo kunakofanywa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ALHAJI MAJID MWANGA. Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Matipwili, BW. GESANDE MWISA amesema amekuwa akipokea vitisho mbalimbali ikiwa pamoja na majaribio kadhaa ya kutaka kuchonganishwa na wananchi kutokana na msimamo wake kuhusiana na utekelezaji wa mpango huo wa kubadilisha mipaka ambao utaathiri zaidi kijiji hicho. BW. MWISA amesema kuwa eneo la mgogoro halitakiwi kuguswa na pande zote mbili mpaka kutakapopatikana muafaka ambao utawezesha kutoa ufumbuzi wa mgogoro husika. Amesema yeye ananshangazwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kuamua kufanya jambo hilo kwa nguvu badala ya kus...

AGIZO LA MKUU WA MKOA KUHUSU MIFUGO PWANI LAPUUZWA

Image

MKUU WA WILAYA BAGAMOYO APINGWA KUTUMIA UBABE

Image

COREFA YAUNGA MKONO VITA DHIDI YA MADAWA KULEVYA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23/02/2017 09:28:28 Chama cha soka mkoa wa Pwani COREFA limeunga mkono kwa kauli moja vita dhidi ya madawa ya kulevya inayoendeshwa na serikali katika kukabiliana na ongezeko kubwa la matumizi ya madawa hayo hatarishi kwa afya za wanadamu. Katibu mtendaji wa COREFA, ABUBAKAR ALLAWI amesema chama hicho kimetambua juhudi za serikali katika kupambana na kadhia hiyo hiyo ambayo imekuwa ni tishio kwa afya na ustawi wa afya za vijana. Amesema COREFA wanatambua matumizi ya madawa ya kulevya yana athari kubwa katika nchi yetu na mpaka sasa yameshapoteza nguvu kazi kubwa tegemeo kwa maendeleo ya nchi. Aidha Katibu mtendaji wa COREFA, ALLAWI amewataka wadau wote wa michezo wanaojihusisha kwa njia moja au nyingine katika utumiaji au uuzaji wa madawa ya kulevya kuacha kufanya hivyo mara moja. END

YPC YATAFUTA MWAROBAINI WA TATIZO LA AJIRA

Image