COREFA YAUNGA MKONO VITA DHIDI YA MADAWA KULEVYA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/23/02/2017 09:28:28
Chama cha
soka mkoa wa Pwani COREFA limeunga mkono kwa kauli moja vita dhidi ya madawa ya
kulevya inayoendeshwa na serikali katika kukabiliana na ongezeko kubwa la
matumizi ya madawa hayo hatarishi kwa afya za wanadamu.
Katibu
mtendaji wa COREFA, ABUBAKAR ALLAWI amesema chama hicho kimetambua juhudi za
serikali katika kupambana na kadhia hiyo hiyo ambayo imekuwa ni tishio kwa afya
na ustawi wa afya za vijana.
Amesema
COREFA wanatambua matumizi ya madawa ya kulevya yana athari kubwa katika nchi
yetu na mpaka sasa yameshapoteza nguvu kazi kubwa tegemeo kwa maendeleo ya
nchi.
Aidha Katibu
mtendaji wa COREFA, ALLAWI amewataka wadau wote wa michezo wanaojihusisha kwa
njia moja au nyingine katika utumiaji au uuzaji wa madawa ya kulevya kuacha
kufanya hivyo mara moja.
END
Comments
Post a Comment