Posts

TFF WAPYA WAPONGEZWA

Thursday, October 31, 2013/Ben Komba/Pwani-Tanzania/17:28:06 Mdau wa soka mkoa wa Pwani ambaye pia ni kiongozi wa vilabu amewapongeza wajumbe wa kamati ya utendaji na Rais wapya   waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania uliofanyika hivi karibuni. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mdau mkubwa wa soka katika Mkoa wa Pwani, BW. MRISHO SWAGALA amewapongeza viongozi wapya waliobahatika kuchaguliwa katika kinyang’anyiro hicho. BW.SWAGALA amefafanua kuwa wanachotakiwa kufanya uongozi mpya ni kutumia fursa hiyo adimu kunyanyua kiwango cha mchezo wa soka nchini ambao umekuwa ukilegalega siku hadi siku kwa sababu ya kukosekana viongozi makini. Aidha ameelezea Jinsi anavyomjua Rais wa sasa wa TFF, JAMAL MALINZI kama ni mchapakazi wa ukweli na amemshuhudia mara kadhaa akitumia uwezo wake wa hali na mali kusaidia mchezo huo hususan katika Mkoa wa Pwani. END.

SUMATRA YAOMBA USHIRIKIANO.

Image

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAENDELEA KULALAMIKIWA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/29/10/2013-09:41 Halmashauri ya mji wa Kibaha imeshauriwa kuangalia njia njia mbadala ya kuhakikisha kuwa pikipiki na wenye magari wanakuwa na maeneo maalum ya kuegesha magari yao. Hayo yamezungumzwa na diwani Kata ya Maili moja, BW.ANDREW LUGANO kufuatia malalamiko ya madereva wa vyombo hivyo kufuatia halmashauri kubandika mabango kuzuia uegeshaji wa magari maeneo mbayo yamezoeleka kwa shughuli hiyo. BW.LUGANO ameongeza kuwa yeye kama diwani wa Kata ya Mailimoja hakubaliani kabisa na hatua aliyochukua Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO wa kutoa tangazo hilo. Bw.LUGANO amemtaka Mkurugenzi kabla ya kuanza kubandika matangazo ya makatazo ya uegeshaji wa magari na pikipiki maeneo ambayo yamezoeleka, angefanya utaratibu wa kutengeneza miundombinu ambayo itasaidia kupunguza tatizo hilo yaani maegesho. Naye dereva wa bodaboda BW. RAMADHAN SAID wa mjini Kibaha ameeleza kusikitishwa kwake na halmashauri kutunga sheria...

SUMATRA NA WANANCHI.

Image
Ben Komba/29-Oct-13/10:36:08 AM Mamlaka way a usafiri wan chi kavu na baharini SUMATRA wamewasisitizia wananchi kuto ushirikiano kwao katika kuhakikisha mazingira ya usafirishaji wa abiria na mali zao unakuwa salama na uhakika. Afisa mwandamizi wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA ameyasema alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha ambapo amesema wamekuwa wanakutana na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. BW.IROGA amesema mara nyingi wamekuwa wakikutana na abiria ambao hawaelewi umuhimu wa magari yao kukaguliwa, kitu ambacho ni jukumu kubwa la SUMATRA katika kuhakikisha vyombo hivyo vya usafiri   vinakuwa katika viwango vinavyostahili kusafirsha abiria na mali zao. Ameongeza kuwa abiria wengi ulalamika kwamba wanacheleweshwa safari zao ambapo wakati mwingine mabasi hayo yakionekana dhahiri ni mabovu, na hivyo kuwataka abiria kuelewa dhana nzima ya SUMATRA ya kukagua magari hayo na kuhakikisha hayak...
Image

WAZAZI WASAIDIANE NA WALIMU

Image

BIG RESULTS NOW

Image