Posts

RAGE AFUNGUA TAWI SIMBVA TISHIO KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Feb-13/18:50:15 Mwenyekiti wa klabu ya Simba maarufu kama wekundu wa Msimbazi amezindua rasmi tawi namba 11 la SIMBA TISHIO lillilopo Katika Mtaa wa Kwa mfipa mjini Kibaha na kuongea na wanachama na washabiki wa timu hiyo mjini Kibaha. Akizungumza katika mkutano huo amewataka wana simba kutoachia klabu hiyo watu wasio na uwezo wa kifedha kutokana na mpira kwa hivi sasa kutawaliwa na fedha, amebainisha uwepo wa gharama mbalimbali ambazo wakati mwingine inakuwa haina uwezo wa kifedha kuzilipa na kama kiongozi unahitajika wakati wote kuwa na jibu muafaka kuhusiana na kila kinachotokea klabuni. Mwenyekiti RAGE amesikitishwa na baadhi ya magazeti ya Michezo kwa kupotosha taarifa mbalimbali kwa lengo la kutaka kuuza magazeti na kuwachanganya wapenzi na washabiki wa soka, akitoa mfano habaria ambayo gazeti moja la michezo nchini lilitoa ya kuwa Malkia wa Nyuki hawahitaji RAGE na KABURU kitu ambacho sio kweli Kabisa. Naye Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM am...

OPERESHENI SENSA 2012.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21 February, 2013/15:59:31 Kikosi namba 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, kimetoa wahitimu 994 wa mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana maarufu kama operesheni sensa 2012 ikiwa ni mhafali ya 102 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo ambapo kati ya wahitimu hao wavulana ni 754 na wasichana 240. Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao AFANDE. MARTIN MABENA, inasema kuna baadhi ya hao vijana walioshiriki mafunzo hayo ya opersheni sensa kuna walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kutokana na sababu za kiafya ni mmoja, vifo wawili, utovu wa nidhamu wawili na kuwa na jumla ya wahitimu watano walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kati yao wavulana wakiwa wawili na wasichana watatu. AFANDE MABENA amesema katika risala hiyo kuwa malengo ya operesheni sensa ni kujenga uzalendo na uvumilivu miongoni mwa vijana wa Tanzania, ikiwa pamoja na kuwaanda kuwa raia wema ili kuwezesha upatikanaji wa viongozi bora watakaoweza kuiilinda nchi na kuitumikia kwa malengo ...

MAJI CHANZO KIBAHA WANAOFAIDIKA NI WA DAR ES SAALAM.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/16-Feb-13/20:23:45 Kukosekana kwa maji ya bomba kwa takriban mwezi mmoja kumesababisha Diwani wa Kata ya Mailimoja mjini Kibaha BW. ANDREW LUGANO kufanya ziara ya ghafla katika ofisi ya DAWASCO katika mkoa wa Pwani kutaka kujua ni nini chanzo cha ukosefu wa maji katika mji huo ili hali chanzo kipo mkoani mwao. Katika Ofisi za DAWSCO tulibahatika kumkuta Meneja wa DAWASCO, BW. ROBERT MUGABE ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tatizo hilo ukapita uamuzi wa meneja huyo ambaye alidai maji jana yake yalitoka kuambatana na diwani huyo kwenda kumuonyesha maeneo ambayo maji kwao sasa ni kitendawili. Baadhi ya maeneo ambayo yalifikiwa na Meneja huyo wa DAWASCO kushuhudia mwenyewe kutokuwepo maji na uhariobifun wa miundo mbinu ambayo DAWASCO wamezembea kufanya ukarabati na wakijua kutofanya hivyo ni kusababisha wateja kukosa huduma hiyo muhimu kwa binadamu. Baadhi ya wananchi wameelezea kukerwa kwao na wasoma mita ambao wamekuwa wakifika majumbani kwao ilihali wakij...

FULL COUNCIL TC

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21-Feb-13/18:38:58 Katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2012/2013 halmashauri ya mji wa Kibaha imefanikiwa kutekeleza na kuimarisha utoaji wa huduma katika kwa ufanisi mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya,usafi wa mazingira, elimu na uimarishaji wa miundo mbinu ya barabara ikiwa pamoja na kununua greda. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO amebainisha kuwa halamshauri yake katika kipindi cha fedha kinachoishia Julai mwaka huu, ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 18 lakini mpaka sasa kiasi kilichokusanywa ni shilingi bilioni nane tu, na juhudi zinafanyika katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa au kuvukwa kwa kubuni vyanzo mbalimbali vya kujikusanyia mapato. BI.OMOLO ameongeza kuwa halmashauri yake imelenga kukusanya mapato hayo katika vyanzo mbalimbali ikiwemomaegesho ya magari, machimbo ya mchanga, kodi za majengo, kodi ya ardhi na msurur wa kodi nyingine mbalimbali kama ilivyoainishwa katika hotuba ya bajeti ...

DailyNews Mobile Edition - State condemns priest’s murder

DailyNews Mobile Edition - State condemns priest’s murder

MKURUGENZI SHIRIKA ASHUTUMIWA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-Feb-13/18:54:49 Kufuatia kupatikana kwa vipeperushi vinavyosemekana vimechapishwa na wafanyakazi wa shirika la elimu Kibaha zenye kushutumu uongozi wa shirika hilo chini ya Mkurugenzi mtendaji BW. CYPRIAN MPEMBA kwa kupendelea baadhi ya wafanyakazi na kuwaweka wengine pembeni. Kipeperushi hicho kilichomfikia mwandishi wa habari hizi kikiwa na malalamiko kadhaa yanayomshutumu Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha kuhusiana na masuala mbalimbali likiwamo kumtaka amuondoe Afisa Tawala wake na kudai kwamba ni mtu anayemshauri juu ya ubaya wa wengine ilihali akificha ya kwake. Mbali ya lawama hizo kipeperushi hicho kilifika mbali kwa kudai mkurugenzi huyo amekuwa akikataa kutoa fursa kwa wafanyakazi kwenda kujisomea kwa madai ya kuwa shirika halina fedha na wakati huohuo anatoa nafasi kwa mfanyakazi mmoja kwenda kusomea PHD kutokana tu na ukaribu wao. Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la elimu Kibaha, DKT. CYPRIAN MPEMBA amesema anachoja...

Members of Congress Demand Obama Administration Classify Ft. Hood Attack an 'Act of Terrorism' - ABC News

Members of Congress Demand Obama Administration Classify Ft. Hood Attack an 'Act of Terrorism' - ABC News