Posts

TANESCO YANUIA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA PWANI.

TANESCO PWANI YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Jan-13/08:23:59 Shirika la umeme katika mkoa wa Pwani linatarajia kufikia wateja elfu 17500 kwenye kipindi cha mwaka 2013-2014 ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafiki wateja wengi zaidi katika lengo la kuwafikia wateja 250,000 nchi nzima sawa na kupunguza bei ya uunganishaji wa huduma hiyo kwa wateja. ... Meneja wa TANESCO mkoa wa Pwani, BW. JOHNSON MWIGUNE amesema shirika hilo lina mikakati ya kurekebisha utoaji huduma, kwa kuhakikisha kuna kuwa na ongezeko la wateja wapya ili kuongeza makusanyo ya kila mwezi ya shirika, na katika kuvutia wateja shirika limeanza kwa kushusha bei ya kuunganisha huduma hiyo kwa wateja wa kawaida hali ambayo inatoa fursa kwa watu wenye kipato cha kati kupata huduma hiyo. BW.MWIGUNE amesisitiza kuwa shirika lake litaendelea na zoezi la ufungaji wa mita za luku kwa wateja wake katika suala zima la matumizi ya digitali na kuachana na Mita za analogia na zoezi hilo limefanikiwa kwa asi...

KIBAHA TC YAPATA GREDA NA GARITAKA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-Jan-13/19:10:34 Halmashauri ya mji wa Kibaha imezindua Greda la kutengenezea barabara na gari la kubeba taka katika suala zima la uboreshaji wa usafi wa mazingira na uimarishaji w mipango miji kutokana na maeneo yote ambayo hayajapasuliwa barabara kutarajiwa kufikiwa. Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI. LEAH LWANJI amebainisha kuwa gari la kubeba taka limetolewa na manispaa ya mji wa GOTLAND kwa ajili ya halmashauri ya mji mara baada ya ujumbe wa viongozi na madiwani kutembelea nchini SWEDEN na wenyeji wao kuwapatia zawadi ya gari hilo ili kusaidia kutunza mazingira ya mji wa Kibaha. BI. LWANJI amesema greda kwa ajili ya kuchonga barabara katika halmashauri ya mji na kukodisha hilo limepatikana kutokana mapato ya ndani ya halmashauri na limegharimu takriban shilingi milioni 528/= za kitanzania, akizungumzia juu ya vitendea kazi vingine kama gllovu, viatu na vinginevyo vimekuja pamoja na gari kwa ajili ...
Image
WAKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA WATAKA SERIKALI IWAAJIRI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-Jan-13/17:31:20 Serikali nchini imetakiwa kuajiri wakalimani katika nyanja mbalimbali ikiwa sehemu ya kutambua uwepo wa walemavu wa kusikia, ambao kutkana na tatizo linalowakabili inakuwa ngumu kwao kupata taarifa juu ya maambo mbalimbali kutokana na kukosa nyenzo za kujimudu ikiwa pamoja na wakalimani. Mwandishi wa habari hizi nimebahatika kuzungumza na Mwanachama wa chama cha Tanzania Association of Sign Language Interpreters (TASLI), au chama cha wakalimani wa lugha ya alama Tanzania, BW. HABIB UPURUTE ambae amesema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingiora magumu kutokana na watu wengi kufikiri kazi hiyo ni nyepesi, na hivyo kuifanya hata serikali kutotupia macho kada hiyo. BW. UPURUTE amebainisha walemavu wa kusikia wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa kunakosababishwa na watu wengi katika jamii kutoifahamu barabara lugha ya alama na hivyo kuchangia kuwanyima fursa mbalimbali...

SERIKALI YATAKIWA KUAJIRI WAKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA.

WAKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA WATAKA SERIKALI IWAAJIRI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-Jan-13/17:31:20 Serikali nchini imetakiwa kuajiri wakalimani katika nyanja mbalimbali ikiwa sehemu ya kutambua uwepo wa walemavu wa kusikia, ambao kutkana na tatizo linalowakabili inakuwa ngumu kwao kupata taarifa juu ya maambo mbalimbali kutokana na kukosa nyenzo za kujimudu ikiwa pamoja na wakalimani. Mwandishi wa habari hizi nimebahatika kuzungumza na Mwanachama wa chama cha Tanzania Association of Sign Language Interpreters (TASLI), au chama cha wakalimani wa lugha ya alama Tanzania, BW. HABIB UPURUTE ambae amesema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingiora magumu kutokana na watu wengi kufikiri kazi hiyo ni nyepesi, na hivyo kuifanya hata serikali kutotupia macho kada hiyo. BW. UPURUTE amebainisha walemavu wa kusikia wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa kunakosababishwa na watu wengi katika jamii kutoifahamu barabara lugha ya alama na hivyo kuchangia kuwanyima furs...

WALEMAVU WA KUSIKIA WAHITAJI WAKALIMANI ZAIDI.

Image
WAKALIMANI WA LUGHA ZA ALAMA WAHITAJIKA KUWASAIDI VIZIWI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Jan-13/18:11:47 Chama kinachofanya utafiti juu ya watu wasiosikia nchini, (TADERE} kimefanya warsha maalum kwa wazazi na walimu wenye watoto walemavu na maofisa watendaji wa vijiji katika kuboresha mazingira ya kijamii kwa watu wasiosikia ambao wamekuwa wakipitwa na mambo mbalimbali kutokana na hali yao. Mkurugenzi wa TADERE, BW. NIDROSY MLAWA amesema watu wenye matatizo ya kusikia wamekuwa wakiachwa nyuma katika masuala mbalimbali kutokana na ukosefu wa wakalimani wa kutosha kuwatafsiria matamko mbalimbali yanayotolewa na serikali na kusababisha ushiriki wao kuwa mdogo kama katika mchakato wa katiba mpya unaooendelea. BW. MLAWA amebainisha jamii lazima ikumbuke kuwa walemavu wa kusikia nao wana wajibu wa kupata huduma za kiroho na hivyo ameshauri wakati sasa umefika kwa madhehebu ya dini mbalimbali kuweka mazingira ambayo yatamuwezesha mtu asiyesikia kupata huduma hiyo ya kiroho. Naye kami...

JUST IN:WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI KIBITI, WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI ~ Father Kidevu

JUST IN:WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI KIBITI, WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI ~ Father Kidevu

DALILI ZA NEON MAJIMAJI, ENZI ZILEEEE

DHARAU HAZITOSAIDIA KUTATUA MGOGORO WA GESI. ~ Father Kidevu