WANANCHI WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI SHIRIKISHI
WANANCHI WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI SHIRIKISHI KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Saturday, 06 January 2018
Wananchi wametakiwa kudumisha dhana ya ulinzi shirikishi katika maeneo yao ili kupambana na vitendo vya uhalifu mjini Kibaha.
Hayo yamezungumzwa na Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi ERNEST SHALUWA, alipozungumza na wakazi wa mtaa wa mkoani katika halmashauri ya mji wa Kibaha ambapo amesema kwa kutumia ulinzi shirikishi kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.
Afande SHALUWA amewaagiza wakazi wa mtaa wa mkoani kuwatambua vijana watakaokuwa tayari kushiri katika suala la ulinzi shirikishi ili waweze kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu, aidha amewataka wakazi hao kuwa na utamaduni wa kupeana namba za simu ili kurahisisha mawasiliano linapotokea tukio la uhalifu katika maeneo yao.
Naye mkazi WILLIAM SHAYO akisoma taarifa ya wakazi hao kuhusiana na matukio ya uhalifu katika mtaa wa Mkoani amesema kumekuwepo na ongezeko kubwa uhalifu katika maeneo yao toka kuhamishwa kwa kituo cha Polisi eneo hilo.
Hivyo wameliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kujenga kituo cha Polisi katika mtaa wa mkoani ili kuweza kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kudumisha hali usalama na amani mtaani hapo.
END
Comments
Post a Comment