Posts

Showing posts from June, 2017

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Image

MAMA ATELEKEZWA KUTOKANA KUZAA WATOTO MAPACHA MFULULIZO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14/06/2017 13:44:19 Mkazi mwanamke ZAINAB HAMIS anayeishi wilaya ya Mkuaranga amejikuta ametelekezwa kufuatia kukimbiwa na mume wake kutoka na kubarikiwa uzazi wa watoto mapacha na kujikuta akiwa na familia kubwa kinyume cha matarajio yake. BIBI. ZAINAB amesema ameolewa na BW. NASIBU KADAMA anayefanya kazi uvuvi ambaye mara ya mwisho alimuaga mkewe anakwenda kutafuta Songosongo lakini mpaka leo hii hajaonekana. BIBI ZAINAB alizaa watoto mapacha wawili wawili mara tatu baadaye akazaa mmoja pekee yake kabla ya kufunga dimba kwa kuzaa watoto watatu kwa mpigo, hali iliyomfanya BW. NASIBU KADAMA kuamua kuitelekeza familia yake na kupotelea kusikofahamika. INSERT END

MLIPUKO WA UGONJWA WA NGURUWE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/06/2017 12:59:37 Halmashauri ya mji wa Kibaha imepiga marufuku usafirishaji na uuzaji wa nguruwe kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe uliotokea katika mji wa Kibaha. Afisa habari, mawasiliano na uhusiano wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.INNOCENT BYARUGABA amesema kumekuwepo na vifo vingi vya nguruwe kati ya kipindi cha mwezi Mei katika kata za Viziwaziwa na Picha ya Ndege ambapo mpaka sasa nguruwe 71 wameshakufa. Na timu ya wataalamu kutoka idara ya mifugo na uvuvi walipofanya uchunguzi wa awali kubaini sababu ya vifo vya wanyama hao  kwa mwonekano na kwa uchunguzi wa wanyama hao waliokufa zilionyesha kuwepo kwa viashiria vya ugonjwa    wa homa ya nguruwe (African swine fever}. INSERT Daktari wa mifugo wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. DEOGRATIUS MGUTE amesema wao kwa upande wao wanaendeleakupita maeneo mbalimbali ya mitaa na kata zote ili kutoa elimu na kusimamia udhibiti wa ueneaji wa ugonjwa huo....

POLISI RUKWA LAWAMANI KUZEMBEA KESI YA MAUAJI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/06/2017 11:35:07 Katika hali inayoashiria kuwa bado baadhi ya watumishi wa Jeshi la Polisi kushindwa kwenda na kasi ya utendaji ya serikali ya awamu ya tano, Polisi katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga wamewaachia huru katika mazingira ya kutatanisha wamewaachia huru watuhumiwa wa mauaji na wao kuendelea na vitisho. Watuhumiwa hao BW.YEGELA SHIGELA na BW.DOTTO PETER ambao awali walimtishia Diwani wa Kata ya Kipeta, BW RASHID DAUD KALELE na hatimaye kufanikiwa kumuua mke wake, BIBI MONICA MASIGANI kwa kumkata na shoka kichwani na kusababisha kifo chake. Tukio hilo limetokea licha ya Diwani huyo kutoa taarifa ya kituo cha Polisi Kata ya Kipeta na kukosa msaada na hata yalipotokea mauaji, Polisi hao waliwaachia huru watuhumiwa na wao kuendelea kutoa vitisho ambapo walimpigia simu saa saba usiku na kumuambia kwamba amewashtaki na wao sasa wapo huru hawatishi kwa lolote. Diwani huyo BW. RASHID DAUD KALELE ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa B...