Posts
Showing posts from May, 2017
WANANCHI WAJITOLEA KUKARABATI KIPANDE CHA BARABARA MLANDIZI
- Get link
- X
- Other Apps
By
BERNARD KOMBA
-
Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/05/2017 15:56:54 Wananchi katika mji wa Mlandizi wamejitolea kutengeneza miundombinu ya barabara iliyoharibika kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa takriban miezi miwili nchini. Wakazi hao wa Mlandsizi Mtongani waliungana kwa umoja kukarabati kipande hicho cha barabara ambacho kilikuwa na kalavati lililozidiwa nguvu na maji yaliyokuwa yananatiririka na kuzidi kiasi cha kupita pembeni na kusababisha kumeguka kwa barabara hiyo inayounganisha vitongoji vya Msagasa na Mtongani. Mmoja wa wakazi wa eneo BW.KONDO MGEGEDA amesema kipande hicho cha barabara kinachounganisha vijiji vya Mlandizi na kuelekea maeneo ya Disunyala na Mzenga kiliharibika katika kipindi cha mvua na kusababisha usumbufu mkubwa kwa magari yaliyotaka kwenda maeneo hayo. Hivyo kwa kuliona hilo wakaamua kuita msaragambo kwa ajili ya kukarabati eneo hilo ili kuwezesha usafiri wa pikipiki kupita maeneo hayo katika kupunguza makali ya tatizo hilo. ...
RAIS MAGUFULI AMWAGIWA SIFA
- Get link
- X
- Other Apps
By
BERNARD KOMBA
-
Ben Komba/Pwani-Tanzania/27/05/2017 09:44:00 Rais JOHN POMBE MAGUFULI amepongezwa kufuatia hatua mbalimbali anazochukua kukabiliana na upotevu wa fedha za mchanga wa madini ambao uliokuwa unaigharimu nchi zaidi ya matrilioni ya shilingi zilizokuwa zinapotea kwenye baadhi ya mikono ya watumishi wa serikali wasio waaminifu. Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE la mjini Kibaha, BW.ISRAEL ILUNDE ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi pembeni mwa jukwaa la ufahamu wa kiraia linalofanyika kila ya ijumaa ya mwisho wa mwezi. Ambapo amesema hatua ambazo amekuwa akizichukua kudhibiti uvujaji wa mapato mbalimbali hazina budi kuungwa mkono na umma wa Watanzania kwani zitawezesha nchi kuelekea katika maendeleo endelevu kwa ustawi wa n chi katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii. Bw. ILUNDE ameongeza kitendo chake cha kutofumbia macho vitendo hivyo ni ishhara tosha ya kuonyesha lengo l...
SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LALAMIKIWA URASIMU MALIPO YA WAKANDARASI
- Get link
- X
- Other Apps
By
BERNARD KOMBA
-
Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/05/2017 09:53:24 Baadhi ya wazabuni wanaofanya kazi na Shirika la Elimu Kibaha wamelalamikia kitengo cha ukaguzi kwa kuwakata fedha ambazo wamepatana kulipwa kwa zabuni wanapewa kwa visingizio ambavyo havina mantiki. Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi kwa takribani wiki mbili kufuatia malalamiko ya mmoja wa wazabuni ambaye alipatiwa kazi ya kufanya matengenezo katika chumba cha kuzalishia dripu za kwa ajili ya wagonjwa, BW.KABUGI MNDEME na baadaye kulipwa nusu ya fedha iliyopo katika makubaliano. BW.MNDEME amesema kuwa yeye aliingia makubaliano ya kuweka milango na madirisha ya aluminium katika chumba hicho cha kuzalisha dripu za maji ya kuongezewa wagonjwa kupitia LPO No. 20161163 ambapo kwa upande wake ametimiza wajibu na kukamilisha matengenezo hayo ambayo gharama yake halisi ilikuwa shilingi 5,892,500.00. BW.MNDEME ameongeza kuwa cha kushangaza mara kazi ilipokamilika ndipo urasimu wa malipo ulipoanza, kukaan...