MVUA ZALETA FARAJA KWA WAKULIMA WA CHAURU


Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/04/2017 11:39:56
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa, Ushirika wa umwagiliaji wa kilimo cha Mpunga halmashauri ya Chalinze unatarajia kupata mavuno makubwa kutokana maadalizi mazuri ambayo wameyafanya kuelekea msimu huu wa kilimo.

Afisa umwagiliaji wa ushirika huo BW.AIDAN MTEGA amesema hayo shambani alipokuwa  anasimamia shughuli za umwagaji mbolea katika mpunga, ambapo amesema kuwa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kwa bei nafuu kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwaa mavuno katika msimu huu wa kilimo.

BW.MTEGA ameongeza kichocheo kingine kikubwa kitachosaidia upatikanaji wa mavuno kwa wi ngi ni kufanikiwa kupatiwa umeme wa REA ambao urahisishaji usambazaji wa maji katika mifereji inayotumika kwa umwagiliaji katika shamba hilo tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kununua mafuta ya kuendeshea pampu ya kusukuma maji.

Ameeleza kuwa wamekuwa wakikabiliwa na chamgamoto mbalimbali katika kusimamia ushirika huo hususan katika miundombinu ya umeme na maji na katika siku hizi za karibuni kumejitokeza kundi la wakulima wanaotaka kuhhujumu kwa makusudi kwa miundo mbinu ya umeme ili kufanya Bodi iliyopo madarakani ishindwe kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Naye mwenyekiti wa ushirika wa kilimo cha umwagiliaji wa mpunga Ruvu, BW. SADALLAH CHACHA kwa upande wake ameainisha changamoto kubwa wanayokabiliana nayo iliyosababishwa na Bodi iliyopita ambayo iliingia mkataba batili na mwekezaji wa Kichina, MS.GUOMING TANG ambaye kwa sasa amekuwa kikwazo kikubwa katika kuharakisha maendeleo ya ushirika huo.

Ambapo sasa imefikia hatua ya mwekezaji huyo kufunga maji kwenda katika baadhi ya mashamba kwa madai ya yeye kuwa na mkataba ambao hautambuliki na sheria za ushirika.
INSERT:MY VOX
INSERT 1:AIDAN MTEGA
INSERT 2:SADALLAH CHACHA

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA