MWANAMKE AKAMATWA AKITOA MAFUNZO YA KIGAIDI KWA WATOTO BAGAMOYO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/06/10/2016
06:04:43
Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani
linamshikilia mwananchi mmoja mkazi wa eneo la
Kimarang’ombe Kata ya Nianjema, Tarafa ya Mwambao Wilaya ya Bagamoyo kwa
kosa kutoa mafunzo yanayohusiana na uhalifu kwa watoto
wadogo.
Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, BOINVENTURE MUSHONGI imemtaja BIBI.ASHURA SAID
ambaye ni Mwalimu wa madrassa ya Al rahma alinasa katika mtego wa Polisi
kufuatia taarifa ambazo walipata kutoka kwa wananchi juu ya vitendo vyake vya kuwapa kasumba ya chuki watoto hao.
Kamanda MUSHONGI ameongeza baada ya kupata
taarifa hizo Polisi walifanya uvamizi wa kustukiza na kumpekua mtuhumiwa huyo
na kufanikiwa kumkuta na bomu moja la moshi lenye namba G2020C SS-STCS katika
makazi yake.
Amebainisha kuwa uchunguzi wa awali
unaonyesha makazi hayo ambayo BIBI.ASHURA SAID alikuwa anaishi ni mali ya
Taasisi ya kiislamuya AKHA LAAGUL ISLAM ambayo imesajiliwa kwa lengo la utoaji
wa huduma kwa watoto yatima katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es saalam,
Tanga na Pwani na kinyume chake wamekuwa wakitumia fursa hiyo kutoa mafunzo ya
kigaidi kwa watoto hao.
Kamanda MUSHONGI amesema mbali ya kukamatwa
kwa mwanamke huyo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata vijana 22 kati yao
16 ni wasichana na 6 ni wavculana walipokuwa wanajaribu kutoroka.
END.
Comments
Post a Comment