USHIRIKIANO WA WANANCHI UNAHITAJIKA KUPAMBANA NA UHALIFU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/30/08/2016 13:10:17
Kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Pwani imefanya kikao na kamati ya amani ya
viongozi wa dini kutathmini hali ya kukosekana kwa amani kunakosababishwa na
majambazi ambao wamejichimbia katika wilaya za Mkuranga na Rufiji.
Mkuu wa mkoa
wa Pwani, MHANDISI EVARIST NDIKILO amesema kuwa mapambano yanaendelea mpaka
sasa katika kuhakikisha wanafuta kabisa mtandao huo wa ujambazi ambao umekuwa
kitisho kikubwa kwa amani na usalama wa wananchi.
BW.NDIKILO
amesema kuwa ni juu ya jamii kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama katika
kusaidiana kwenye udhibiti wa vitendo vya uhalifu na hasa ikizingatiwa
wanaofanya hivyo ni ndugu zetu au majirani zetu.
Ametoa mfano
wa kijana Fundi seremala ambaye alimuua Mwenyekiti wa kijiji cha PANZUA ambaye
aliishi katika kijiji hicho kwa takriban miaka 25, lakini kwa mshangao wa wengi
alichukua hatua ya kumuua mwenyekiti wa kijiji.
Aidha ametumia
fursa hiyo kutoa onyo kuhusiana na maandamano yanayotaka kufanyika Septemba 1
kwa kuyaita kuwa hayana tija na yamepigwa marufuku na serikali na hivyo ni
vyema wananchi wakatii sheria bila shuruti.
END
Comments
Post a Comment